SERIKALI YASHAURIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATANZANIA WAISHIO NJE YA TANZANIA KATIKA UWEKEZAJI.

 

images

Na Waandishi wetu-MAELEZO_Dar es Salaam.

…………………………………………………………….

 

 Kamati ya  Bunge  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa imeshauri Serikali kutoa fursa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuja kuwekeza  nchini katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wetu.

 Kauli hiyo imetolewa
(leo) na wajumbe wa Kamati hiyo ilipokutana na viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya bajeti ya mwaka 2013/2014

 Walisema wakati umefikwa kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kutowekewa vikwazo katika kupata taarifa muhimu  zinazohusu sekta mbalimbali za uchumi ili waweze kuja kuwekeza badala ya fedha zao kukaa nazo nje ya Tanzania.

 Waliongeza kuwa ni vema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikaunda Kitengo maalum cha diplomasia ya uchumi kitakachoshirikisha  wataalamu wa sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utangazaji wa fursa za uwekezaji nchini kwa ili kuboresha nyanja za uchumi kupitia Watanzania waishio nje.

 Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati hiyo Naibu Waziri wa Wizara wa Mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Maalim alisema kuwa Serikali hivi sasa inaendelea kutangaza fursa mbalimbali ambazo zipo Tanzania ambapo tayari wawekezaji kutoka Oman wameshaonyesha nia ya kuwekeza nchini.

 Alisema kuwa wawekezaji hao wanakusudia kununua nyama ambapo pia watajenga machinjio ya kisasa ambayo yatatumika kuchinjia mifugo kabla ya nyama haijasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s