Rais Kikwete amkaribisha Rais Uhuru Kenyatta Arusha


 

8E9U0184Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro wakati alipowasili jana jioni kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wan chi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki unaofanyika jijini Arusha. 8E9U0327Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mkewe Margareth Kenyatta wakifurahia ngoma za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijijini Arusha(picha na Freddy Maro) 8E9U0339Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mkewe Margareth Kenyatta wakifurahia ngoma za utamaduni muda mfupi bbada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijijini Arusha(picha na Freddy Maro) 8E9U0364Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mkewe Margareth Kenyatta wakifurahia ngoma za utamaduni muda mfupi bbada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijijini Arusha(picha na Freddy Maro)

Tamasha la Kihistoria la Makabila ya Sukuma na Kerewe, linalohusu Vyakula vya Asili, Ngoma na Tamaduni za Makabila hayo, linalotarajiwa kufanyika CCM Kirumba Mwanza na Uwanja wa Mongella Ukewrewe wiki hii


 

 

 

Mkurugenzi Msaidizi wa My Way Entertainment, Rose Mwita(Kulia) akifafanua jambo kuhusiana na Tamasha la Kihistoria la Makabila ya Sukuma na Kerewe, linalohusu Vyakula vya Asili, Ngoma na Tamaduni za Makabila hayo, linalotarajiwa kufanyika tarehe 27 CCM Kirumba Mwanza na Tarehe 28 Uwanja wa Mongella Ukewrewe Mwezi Huu, Kushoto ni Afisa Habari wa Kampuni ya My Way Entertainment, Osbert Chusu,(Picha Kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).Pia unaweza kubonyeza…http://Wwwmasterkif.blogspot.com

LADY JAY DEE: “NAAMINI KABISA MUNGU SIO RUGE WALA KUSAGA. ATANISMIAMIA KWENYE HILI #CONFIDENCE.”


 

 

 

 

 

 

 

Baada ya mafumbo mengi na vijembe huko twitter na bbm hatimaye mwandana komandoo na super star Lady Jay Dee ameamua kufungua na kutaja majina ya hao watu wenye beef nae kupitia ukurasa wake wa twitter. Jide amefungua na kupodt yafuatyao. 

 

 

 

 

 

Pia unaweza kubonyeza…http://Wwwmasterkif.blogspot.com

Wanasiasa hawa hawana shukurani vinywani mwao – Rais Kikwete.


 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewashangaa baadhi ya wanasiasa ambao amewaeleza kuwa hawana shukurani vinywani mwao na wala hawana macho ya kuona mafanikio ya dhahiri ya Serikali katika sekta mbali mbali ikiwemo ile ya barabara na ujenzi wake nchini.

 

Zaidi, Rais Kikwete amewashangaa baadhi ya wanasiasa wa Mikoa ya Kusini ambao wamekuwa wanalalamikia kutokumalizia kwa kipande kifupi cha barabara la Somanga-Nyamwage kuwa ni kushindwa kutimizwa kwa ahadi za Rais Kikwete.

 

Akizungumza juzi, Jumamosi, Aprili 13, 2013 katika Kijiji cha Kasera, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga wakati wa uzinduzi wa Barabara ya lami ya Tanga-Horohoro yenye kilomita 65.14, Rais Kikwete alisema:

 

“Hakuna mtu yoyote ambaye haoni kuwa barabara hii ni ukombozi mkubwa wa wananchi ambao huko nyuma hawakuwa na barabara ya lami, isipokuwa wale wenye macho lakini wanajifanya hawaoni. Hawa ni watu wenye hiana mioyoni mwao na hata Serikali ifanye nini wataendelea kuimba santuri yao ambayo sasa imewachosha watu.”

 

Aliongeza Rais Kikwete: “Wapo watu wanaoendelea kudai kuwa hakuna kilichofanyika. Hawa ni sawa na wale watu wawili ambao walikuwa wanapoteza muda wake kubishana mchana kweupe kuhusu kile walichokuwa wanakiona juu yao kama ni Jua ama Mwezi. Ni wapuuzi tu.”

 

Kuhusu malalamiko ya baadhi ya wabunge wa Mikoa ya Kusini juu ya Barabara ya Lindi-Kibiti na hasa sehemu ya Nyamwage-Somanga, Rais Kikwete alisema:

 

“Hawa ni watu ambao hawana hata shukurani vinywani mwao. Hapa ni mahali hapakuwa na barabara kabisa wala Daraja lile la Mkapa. Wakati Mzee Mkapa alipojenga Daraja la Mkapa wakamkejeli kuwa alichokuwa amefanya ni sawa na kumnunulia shati mzazi wake aliye uchi. Atatoka vipi nje na shati tupu?”

 

“Tulichofanya sisi ni kujenga barabara yote hii ya lami kutoka Lindi hadi Kibiti. Hii ilikuwa ni barabara iliyokuwa haipitiki wakati wa majira fulani fulani. Tumemaliza kuijenga yote isipokuwa kilomita 9.5 ambazo nazo wanamalizia. Sasa watu hawa, wanasiasa hawa wanataka tuwafanyie nini? Barabara haikuwepo kabisa na zimebakia kilomita 9.5 tu na bado wanalalamika na kusema Serikali gani hii? Wanataka tufanye nini?”

 

Wiki iliyopita Bungeni Dodoma Mbunge mmoja wa Viti Maalum wa Chama cha CUF alidai kuwa ahadi ya Mheshimiwa Rais Kikwete kujenga Barabara ya lami ya Lindi-Kibiti ilikuwa haitekelezwi kwa sababu ya kutokamilika kwa sehemu ya Somanga-Nyamwege. Mbunge huyo aliungwa mkono na wabunge kadhaa kutoka Mikoa ya Kusini.

 

Rais Kikwete pia amekumbushia kuwa katika miaka saba tu, Serikali yake imekomesha aibu ya watu wanaokwenda  sehemu moja ya nchi kulazimika kupitia nchi jirani ili wafike.

 

“Tumesahau kuwa miaka michache tu iliyopita watu wa kwenda Mwanza na Musoma walikuwa wanapitia Nairobi na Kisumu katika Kenya? Watu wa kwenda Bukoba walikuwa wanapitia Nairobi, Kampala, Masaka ndiyo wafike Mutukula kuingia Tanzania? Tumesahau haya katika muda mfupi tu wa miaka saba?”

 

Barabara ya Tanga-Horohoro ni moja ya miradi mingi ya miundombinu ambayo inajengwa chini ya ufadhili wa Mpango wa Millenium Challenge Account (Tanzania) wa Shirika la Millenium Challenge Corporation (MCC) wa Marekani.

 

Ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Sh. Bilioni 75.715 ambazo zilikuwa ni pamoja na fidia kwa nyumba na mali nyingine za wananchi pamoja na ujenzi wa misikiti mipya kuchukua nafasi ya misikiti iliyovunjwa kupisha barabara.

 

 

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

 

Ikulu.

 

Dar es Salaam.

 

15 Aprili, 2013

MAMA WEMA AMFANYIA VURUGU WEMA


 

 

 

Na Musa Mateja
NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali, Ijumaa limeinyaka.

 

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.
“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.
Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI. Kwa habari zaidi soma Magazeti Pendwa ya Global yajayo.

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA PROFESA WAMBALI


 

 

IMG_1429Waziri Mkuu,MizengoPinda  akisalimiana na baadhi ya wahadhili katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati aliposhiriki katika  kuaga mwili wa aliyekuwa mhadhili wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wakili Maarufu, Profesa Michael Wambali Chuo Kikuu cha Dar es salaam Aprili 8,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

IMG_1431Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa aliyekuwa mhadhili wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wakili Maarufu, Profesa Michael Wambali Chuo Kikuu cha Dar es salaam Aprili 8,2013. Aliyesimama kushoto kwake ni Mkamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Lwekaza Mukandala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_1443Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa aliyekuwa mhadhili wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wakili Maarufu, Profesa Michael Wambali Chuo Kikuu cha Dar es salaam Aprili 8,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_1447Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na waombolezaji wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa aliyekuwa mhadhili wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wakili Maarufu, Profesa Michael Wambali Chuo Kikuu cha Dar es salaam Aprili 8,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

IMG_1450Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na waombolezaji wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa aliyekuwa mhadhili wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wakili Maarufu, Profesa Michael Wambali Chuo Kikuu cha Dar es salaam Aprili 8,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

…………………………………………………………………………..

 

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, na wakili maarufu Profesa Michael Wambali ambaye alifariki dunia Aprili 4, 2013 katika hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali ya gari.

 

 Shughuli ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Profesa Wambali ilifanyika leo asubuhi (Jumatatu, Aprili 8, 2013) kwenye ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kupelekwa kanisani kwa misa maalum.

 

 

 

Akizungumza na waombolezaji hao kabla ya kutoa heshima za mwisho, Waziri Mkuu alisema mchango wa Prefesa Wambali kwenye fani ya sheria ni mkubwa mno na hauelezeki. “Kama walimu wenzake wangeamua kuhesabu idadi ya wanafunzi ambao Profesa Wambali aliwafundisha, ni dhahiri kuwa idadi yao ingekuwa kubwa kuliko tunavyoweza kufikiria,” alisema.

 

 

 

“Juzi tu tarehe 29 Machi, ametimiza miaka 59 ya kuzaliwa na siku sita baadaye akaaga dunia, lakini katika kipindi cha miaka yake 59 ni miaka 32 ambayo aliitumia hapa chuoni. Hapa tulipo wapo Majaji, Mawakili wa Serikali na wa kujitegemea, mahakimu na wengine wako mikoani wameshindwa kufika hapa leo… lakini wote hawa wamefundishwa na Prof. Wambali katika kipindi cha miaka 32 aliyokaa hapa chuoni,” alisema.