Pima ubora wa matumizi ya wavuti yako. (Website Usability Test )

 

 

Tumekuwa tukiandika sana juu ya umuhimu wa kuwa na Wavuti, hivyo kama kusikia wengi tayari wameshasikia na kuelewa umuhimu wake. Siku hizi kuwa na wavuti sio tatizo tena na si suala linalohitaji utaalmu wa kutisha, ila kuwa na wavuti inayofanya kazi, bado kutanendelea kuwa ni sehemu inayohitaji umakini wa kina. Hivyo  leo hii nitagawana nayi machache ambayo kwa njia moja au nyingine yanaweza kukusaidia kuboresha utendaji wa wavuti yako.

 

Kwa wale ambao wanajishughulisha na utengenezaji wa wavuti, au programu yoyote watakuwa wanafahamu, sehemu ngumu na inayotumia muda kwa sana ni sehemu ya kupangilia mfumo na umbo la wavuti au programu. Hii ndio sehemu muhimu inayounganisha umbo la nje na lile la ndani la programu. Kushindwa kupangilia vyema mfumo huo, inamaanisha kuwa na programu isiyo na ushirikiano hivyo haitoweza kufanya kazi zake kama inavyotakikana.

Hivyo, kama hauna uhakika kama wavuti au programu yako imefikia viwango, fuatana nami katika vidokezo vya upimaji wa ubora;

1. Upatikanaji.

Sehemu muhimu na ya kwanza kuzingatia ni upatikanaji wa wavuti yako. Unaweza kuwa hodari wa kufanya matangazo na kugawa vipeperushi vya wavuti yako lakini siku ya mwisho watu wanapotembelea wanakuta wavuti haipatikani au haielewekei. Nimewahi kusema mara nyingi, watumiaji wa wavuti huwa wanachungua (scan) tena kwa sekunde chache mno, hivyo wewe kama mmiliki unahitaji kuhakikisha unatumia hizo sekunde chache kuwashawishi kuendelea kubaki kwako.

Hivyo kwenye hili unatakiwa kuzingatia yafuatayo.

 

 

 

Je wavuti yako inaonekanika vyema kwenye browser zote?

 

Ingawa ni kitu kigumu sana kuhakikisha wavuti inaonekana sawasawa kwenye browser zote, ila ni kitu cha lazima kuhakikisha inaonekana VYEMA kwenye browser hizo. Kama umeshindwa kuhakikisha muonekano mzuri kwenye browser zote, tumia Google Analytics kujua browser inayotumiwa naje watembeleaji wengi wa wavuti yako. Kwa kujua hili, utaweza kufanya maboresho ya muonekano kwenye hiyo browser kama chaguo la kwanza na nyingine zinafuata. Tembelea Browsershot kwa ajili ya kufanya majaribio ya muonekano.

 

 

 

Spidi ya ufungukaji wa wavuti yako ni ya kuridhisha?

 

Hakuna kitu kinachokimbiza watembeleaji kama wavuti iliyo taratibu, niwatembeleaji wachache mno ambao wapo tayari kusubiri wavuti yako iliyo taratibu, hivyo hakikisha muda unaotumia hadi kufunguka kwa wavuti yako ni muafaka. Tumia Pagespeed kwa ajili ya kupima spidi na ushauri wa uboreshaji wake.

 

 

 

Je wavuti yako inapatikanika kwenye mitambo ya utafutaji (Search Engine)

 

Kuna baadhi ya muda unaweza kuona wavuti yako imepata chati na kuwa juu kwenye mitambo hii, ghafla imepotea. Kuna mambo mengi yanaweza kusababisha hili kama kuvamiwa hivyo
ambapo wavuti yako ikatumika kutuma minyoo. Ili kuhakikisha utendaji wa wavuti yako nenda Spider Simulator kupima ubora wa wavuti yako kwenye mitambo ya utafutaji.

 

2. Utambulisho wa chapa (Brand Identity)

 

Watu wengi wamezoea kuwa unapozungumzia ubora wa matumizi ya wavuti ni ni mfuomo na utendaji tuu, hili si kweli. Ubora wa utumiaji pia huzingatia ni jinsi gani watumiaji wanaweza kutofautisha wavuti yako na nyingine. Utofauti huu sio tu wa makala, bali pia kimuonekano. Leo hii ukitembelea tu Facebook, unajua hii ni Facebook, hii husaidia mambo mengi likiwemo la usalama kwa kuwaepusha watembeleaji wako na wavuti bandia. Kwenye hili unatakiwa kuzingatia yafuatayo;

 

 

Je logo na rangi za wavuti yako zinatosha kujitofautisha?

 

 Kama ambavyo nimeshadokeza hapo juu, siku hizi wavuti nyingi hutengenezwa kwa kutumia mitambo ya kuongoza yaliyomo (CMS) ambayo huwa inafanana. Hivyo hupelekea wavuti nyingi kuwa na muonekano ulio sawa. Kutokana na uvivu au kutokuwa na maarifa ya kutosha kwa watengenezaji, wengi huacha muonekanao kama ulivyokuwa mwano, ama iwe kwa kutumia template ya awali ama kwa kununua template ambayo pia huweza kununuliwa wengine. Ukitaka kuhakikisha hili, tembelea wavuti nyingi za nyumbani utagundua mfanano wao wa kimuonekano hivyo hupoteja upekee.

 

Kama umeamua kutumia wavuti kama sehemu ya kazi, hili nitatizo, ila kama ni kwa ajili ya majaribio ama sehemu ya kujifurahisha, basi waweza kupuuzia hili.

 

Menyu:
Menyu ni kama mlango ambao unawawezesha watumiaji kwenda kwenye vymba vilivyomo kwenye wavuti yako. Hivyo unatakiwa kuzingatia kuwa na menu inayojieleza bila kuwachanganya watembeleaji. Epuka kuwa na menyu zinazofanana au zisizofanya kazi kwani kwa kufanya hivyo sio tu utakuwa unawachanganya watembeleaji bali pia utakuwa unawafanya wapotelee hewani.Kwenye menyu, Unatakiwa kuzingatia yafuatayo;

 

 

 

Usiwafanya wakokotoe;
Ukiwa ni mlango wa kuingia sehemu mbalimbali za wavuti yako, usiwafanye waanze kuuliza, eti ni wapi ndio mlango, jaribu kuuliza watu wako wa karibu juu ya mpangilio na lugha uliyotumia na je urahisi wake kuifahamu menyu.Kumbuka, menyu ni mlango, hivyo usiweke mlango usiofunguka au wenye rangi sawa na ukuta, watembeleaji hawatoweza kutofautisha wapi ni mlango, wapi ni ukuta.

 

 

 

Je tovuti(links) za muhimu zinatambulika

 

Usingependa watembeleaji waanze kuhangaika eti anatafuta linki fulani, jaribu kuweka linki muhimu kwenye kurasa ya mbele tena kwa kutumia mtindo mwanana na wenye kujionesha. Lakini, uwekaji huu usipitilize, kwani muhimu zina ukomo. Leo hii ukitembelea blogu nyingi za kitanzania, unakaribishwa na matangazo (muhimu) ila kwakuwa muhimu yamekuwa mengi, kinachotokea ni keri kwa watembeleaji, hivyo siku ya mwisho, watembeleaji huwa wanakokota (scroll) kurasa mpaka kunapoanza makala. Hivyo basi kwa hawa watangazaji, sijui kama wanafikia lengo la kutangaza kwao na ule umuhimu umepotea.

 

Ni mategemeo yangu makala hii itakuwa na msaada kwa jamii, ukiwa na maswali ama ushauri, acha maoni yako hapa.Chanzo:mjengwablog

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s