Bayern yaiangamiza Barca, Champions League

 

 

 

Mashabiki wa Bayern Munich walisherehekea kipigo cha pili katika muda wa siku tisa dhidi ya timu ya Barcelona iliyotamba na usakataji wake wa soka katika bara la Ulaya na pengine dunia, ilipokubali kipigo cha mabao 3-0.
 
Bayern Munich's players celebrate their victory at the end of the UEFA Champions League semi-final second leg football match FC Barcelona vs FC Bayern Munich at the Camp Nou stadium in Barcelona on May 1, 2013. Bayern Munich won the match 3-0. AFP PHOTO / LLUIS GENE (Photo credit should read LLUIS GENE/AFP/Getty Images)
Barcelona ilichezea kipigo cha mabao 4-0 mjini Munich Jumanne iliyopita na kipigo cha jana (01.05.2013), kinaashiria kuwa huenda utandazaji wa soka wa kile kinachojulikana kama ” tiki taka” , unaelekea ukingoni.
 
Bayern Munich ilivamia ngome ya Nou Camp na kufanikiwa kupata nafasi ya kuingia katika fainali ya kwanza ya timu mbili za Ujerumani katika kinyang’anyiro cha Champions League. Bayern imekamilisha hatua hiyo kwa kipigo cha jumla ya mabao 7-0 dhidi ya barcelona, na kuingia katika daraja la kuitwa wafalme wapya wa Ulaya.
 
Wazee wa Tiki Taka Barcelona wakitoka uwanjani vichwa chini na mikoni viunoni
 

Wazee wa Tiki Taka Barcelona wakitoka uwanjani vichwa chini na mikoni viunoni

 
Mabingwa hao wapya wa Bundesliga , ambao wanafukuzia ubingwa wao wa tano katika mashindano hayo ya bara la ulaya , watapambana na Borussia Dortmund hapo Mei 25 katika uwanja maarufu wa Wembley mjini London.
 
Messi aduwaa
 
Nyota wa Barcelona Leonel Messi alikuwa akitazama tu akiwa benchi wakati Bayern ilipokamilisha dhoroba yake na kuwasambaratisha mabingwa hao watarajiwa nchini Uhispania kwa mabao 3-0.
 
epa03684152 FC Barcelona's Argentinian striker Lionel Messi sits on the bench during the UEFA Champions League semi final second leg soccer match between FC Barcelona and Bayern Munich at Camp Nou in Barcelona, Spain, 01 May 2013. EPA/ANDREU DALMAU
 

Leonel Messi akitumbua macho tu bila kujua la kufanya

 
Kwa kumuweka benchi mfungaji wao huyo maarufu baada ya kupata maumivu ya paja , Barcelona walishindwa kuipa changamoto ya maana Bayern, na kushindwa kufurukuta kuweza kupindua matokeo ya hapo awali ya mabao 4-0 mjini Munich.
 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s