SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO KWA WAKUU, WAMILIKI WA SHULE NA VYUO

 

 

 

 

JK-PIc

Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wakuu na wamiliki wa shule na vyuo binafsi kwa minajili  ya kuboresha sekta ya elimu haoa nchini.
Akizungumza  na viongozi wa TAMONGSCO Rais Kikwete amesema sekta binafsi ina mchango mkubwa wa kuinua elimu hapa nchini hivyo jitihada za pamoja zinahitajika katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza
Rais Kikwete aliwataka wamiliki na wakuu wa shule na vyuo binafsi kupunguza ada  kubwa wanazotoza kwa wanafunzi ili watanzania wengi hasa wa kipato cha chini waweze kupata fursa ya elimu.
Aidha Mheshimiwa Rais alisema serikali iko katika Mchakato wa kutunga Sera Mpya ya Elimu baada ya ile ya mwaka 1995, umefikia katika hatua za mwisho na kinachosubiriwa sasa ni maoni ya Wabunge ili Sera hiyo ikamilishwe na kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.
Wakati huo huo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania itaanza maandalizi ya kupitia upya mitaala ya elimu nchini ili nayo ilingane na malengo ya Sera Mpya ya Elimu,mahitaji ya maendeleo nchini na duniani kwa ujumla.
Licha ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu imeongeza sekta hiyo ambapo kuna wanafunzi zaidi ya milioni nane katika shule  za msingi,zaidi wanafunzi milioni moja na laki nane  kwa shule za sekondari na zaidi ya laki moja na sitini elfu kwa upande wa vyuo vikuu.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s