Tanzania kupanua wigo wa kodi kwa njia ya risiti za elektroniki

 

 

 

Na Deodatus Balile, Dar es Salaam
 
Serikali ya Tanzania inatarajia kukusanya shilingi bilioni 600 (dola milioni 370) kwa mwezi baada ya mpango mpya wa kodi kupanua matumizi ya mashine za usajili wa kodi kwa elektroniki (ETR) zitakazoanza kutumika tarehe 15 Mei.
 
Ikiwa mpango huo mpya wa kodi utaonekana kufanikiwa, vituo vya mafuta nchini kote vitatakiwa kutoa risiti za kodi zilizosajiliwa kwa njia ya elektroniki. Juu, muonekano wa kituo cha petroli cha TSN katika Barabara ya Bagamoyo jijin Dar es Salaam. [Na Deodatus Balile/Sabahi]
 
Kwa sasa, serikali inakusanya shilingi bilioni 400 (dola milioni 250) za kodi kwa mwezi.
 
Mashine za ETR huorodhesha risiti za mauzo wakati wa kufunga biashara kila siku na kupeleka data kwa njia ya elektroniki kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya tathmini sahihi ya kodi.
 
“Katika mfumo huu mpya, biashara ambazo hupata idadi yoyote ya fedha kuanzia shilingi milioni 14 (dola 8,600) hadi shilingi milioni 40 (dola 25,000), kuanzia sasa zitatakiwa kutumia mashine za ETR,” alisema Naibu Kamishna wa TRA kwa Mapato ya Ndani Generose Bateyunga. Huko nyuma, biashara hizi ziliweza kukisia tu kodi zao.
 
Bateyunga aliiambia Sabahi kuwa kiasi cha walipa kodi 200,000 wamekuwa wakikwepa kulipa kodi au kulipa kiwango cha chini, na kuongeza kwamba misaada kutoka kwa wafadhili imekuwa ikipungua, kwa hivyo Tanzania lazima ipanue wigo wake kwa ajili ya kugharamia maendeleo.
 
Mashine za ETR zimeunganishwa moja kwa moja kwa intaneti na Mamlaka ya Mapato Tanzania na zinaweza kutoa hesabu za risiti za mauzo ya kila siku. [Deodatus Balile/Sabahi]
 
Mwaka 2010, wakati Tanzania ilipoingiza mashine za ETR, ukusanyaji kodi uliimarika kwa asilimia 9.6 kwa mwaka wa fedha 2010-2011 na asilimia 23 kwa mwaka 2011-2012. “Tunatekeleza awamu mbili, ambazo zitawajumuisha hata walipa kodi zaidi,” alisema.
 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s