WAKATI MWINGINE WANAWAKE HUKOSEA BILA KUJUA!-2

KUKOSEA ni kujifunza. Ukifanya kosa na kutambua, bila shaka huwezi kurudia tena na kama ikitokea hivyo utakuwa umekusudia. Hapa nazungumzia makosa ambayo hufanywa na wanawake bila kujua.

Wiki iliyopita nilieleza baadhi yake, leo nahitimisha katika vipengele vingine. Rafiki zangu, wanaume hawawapendi kabisa wanawake ambao wanawasema vibaya wanawake wenzao.
Hapa kuna aina mbili, kuwateta au kuwaita majina yenye maana mbaya na yanayodhalilisha. Utakuta mwanamke amekaa na mumewe anathubutu kuwaita wenzake majina kama changu, malaya, dadapoa, mhuni, mlupo na mengine yanayofanana na hayo.
Tabia hii haipendezi na unafanya mwanaume wako akufikirie vibaya na inawezekana nawe ni aina ya wale wanawake wenye ‘mdomo’ sana. Tafakari hili.

UZUNGU MWINGI…
Kupenda kumshika kimahaba, kumkumbatia au kuwa naye kimapenzi zaidi mbele za watu, kunamfanya mwenzi wako aone kama umepungukiwa tabia njema. Kwa tafsiri ya haraka, ataona huna staha.
Kujionesha mbele za watu mkifanya mambo yanayoashiria mapenzi, kunawapunguzia heshima na pengine mtaonekana kama wahuni tu na siyo wenzi mnaotumia akili wenye ndoto njema za baadaye.

KIPAUMBELE KUHUSU NGONO
Wanawake wengi wanaharibiwa na hisia kwamba wanaume wapo nao kwa ajili ya mapenzi (ngono) tu! Kwamba, silaha ya mwisho katika mapenzi yao ni kukutana faragha! Hii si kweli.
Wanaume wanapenda wanawake makini, ambao wapo nao kwa ajili ya maisha zaidi. Wanaowaza mambo ya maisha na siyo ngono. Mbaya zaidi, hawapendi kabisa uoneshe kwamba unajua ‘hapindui’ kwako kwa sababu unampatia faragha.
Kumbuka ngono inawezekana kupatikana kwa njia yoyote lakini si amani na mustakabali mzuri wa maisha ya baadaye.

SULUHU YA MIGOGORO
Mwerevu ni yule anayegundua kwamba amekosea halafu anaanza upya kutafuta njia za kutoka kwenye makosa. Huu ndiyo werevu. Siku zote mwanamke mwenye busara na nia njema na uhusiano wake, hapendi kumkosea mpenzi wake na hata kama akifanya hivyo, anakuwa mwepesi sana wa kutafuta njia za kuweka sawa uhusiano wao.
Sifa ya kumaliza migogoro mapema ni bora sana. Wanawake wengine hawaoni kama lina umuhimu mkubwa. Hili ni kosa kubwa.

UMENIPATA RAFIKI?
Mapenzi ni kujifunza na pia unatakiwa kufahamu kwamba hakuna mbabe wala mjinga wa mapenzi. Ukijua kosa lako, utajirekebisha na kuboresha uhusiano wako, wakati ukitafuta elimu zaidi juu ya mapenzi.
Makosa haya usikubali kuyafanya tena, badilika huku ukiendelea kujifunza zaidi. Kuna mjanja kama wewe? Wiki ijayo nitakuwa tena hapa kwa mada nyingine. 

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika Vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s