MWANAUME ALAZWA WODI YA WANAWAKE

Stor: Imalda Mtema

Katika hali ya kushangaza, mwanaume mwenye asili ya Kiarabu  aliyetambulika kwa jina la Karina Mohamed (20), aliwaacha midomo wazi madaktari, wauguzi na wagonjwa wa Hospital ya Amana, jijini Dar baada kulazwa katika wodi ya wanawake akidhaniwa ni mwanamke.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mgonjwa huyo alilazwa hospitalini hapo Aprili 24, mwaka huu ambapo alifikishwa na dada mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja huku akiwa hajitambui, akiwa amevalia mavazi ya kike hivyo madaktari kuamua kumlaza katika wodi ya wanawake.
Chanzo chetu kilizidi kueleza kwamba baada ya mgonjwa huyo kupelekwa wodini, hakuna hata mgonjwa mmoja aliyeweza kumtambua kuwa ni mwanaume kutokana na maumbile yake kufanana kabisa na ya kike lakini wakati madaktari wakiendelea kumhudumia, Aprili 25 akafariki dunia.
Imeelezwa kuwa baada ya kuzidiwa sana, mhudumu wa hospitali hiyo alipotaka kumuwekea mpira kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo ndipo aliposhtuka baada ya kubaini kuwa ana jinsia ya kiume tofauti na alivyodhania.
“Kitendo kile kilimshangaza sana muuguzi huyo na kudondosha kila kitu alichokuwa nacho mkononi huku akisema: Huyu mgonjwa mwanaumeee jamani.”
Mara baada ya waandishi wetu kupewa taarifa, walifika hospitali hapo na kuonana na katibu wa hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Tunu Mwachali ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa suala hilo lipo mikononi mwa polisi.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo Aprili 24, mwaka huu na kulazwa wodi namba 2 ya wanawake na kufariki dunia akiwa anapatiwa huduma na kuongeza kuwa ndugu zake bado hawajafahamika ila jeshi linaendelea na uchunguzi.Chanzo:www.globalpublishers.info

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s