PENNY: NAMSHANGAA DIAMOND, MIMBA IPI KWANZA?


Stori:Mwaija Salum na Joan Lema
HIVI karibuni, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliripotiwa na gazeti moja la Global Publishers akisema demu wake ambaye ni ‘prizenta’ wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ana ujauzito wake na kwamba amemnunulia ‘mkoko’ (gari) la mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kwenda nalo kliniki, Penny ameifungukia kauli hiyo.

Akizungumza na mapaparazi wetu kwa njia ya simu jijini Dar juzikati, mrembo huyo alionesha hali ya kupaniki huku aking’aka na kushangazwa na habari hizo za ujauzito.

Alisema amekuwa akisoma habari za ‘mimba’ yake kupitia magazeti lakini hajaulizwa na mwandishi yeyote, jambo linalomshangaza sana.
Alipoambiwa kwamba aliyesema habari kwamba yeye ana mimba ni Diamond, Penny alisema: Namshangaa! Ni mimba ipi kwanza?
Alikwenda mbele zaidi kwa kusema mbali na madai ya mimba, lakini pia uhusiano wake na msanii huyo unamnyima raha kutokana na maneno ya watu.
Baada ya waandishi kujitambulisha, mahojiano yalikuwa hivi:
Funguka: Vipi, ujauzito unaendeleaje? Ni kweli una mimba ya Diamond au umeshaitoa?
Penny: Mh! Yaani sijui hata niseme nini, nashangazwa sana na hizi habari, nazisikia tu halafu mimi mwenyewe mhusika sijapewa nafasi ya kuzungumza.
Unajua sijazoea maisha haya ya kila wakati kuzungumza na waandishi. Naomba mniache, nani aliwaambia kuwa mimi nina mimba?
Funguka: Diamond.
Penny: Kama ni Diamond muulizeni yeye mwenyewe! Mbona nakosa raha jamani?
Funguka: Vipi mna mpango wa kuoana na Diamond?
Penny: (kwa hasira) Hizo ni ishu zangu binafsi, kama tutaoana au hatuoani ni mipango yetu, sioni sababu ya kutangaza kwenye media.
Funguka: Unaichukuliaje kauli ya mama mkwe wako, yaani mama Diamond? Inadaiwa alisema hatambui uhusiano wowote wa mtoto wake na mwanamke mwingine hadi atakapofunga ndoa.
Penny: Tafadhali sana, sitaki kuzungumzia habari kuhusu mama Diamond. Kwa hilo ‘no comment.’
Funguka: Vipi lakini, unainjoi kuwa na uhusiano na Diamond?
Penny: (Akakata simu).
Funguka: Haloo… haloo!
Hata hivyo mapaparazi wetu walipojaribu kumpigia simu tena hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu mpaka kukatika yenyewe.Chanzo:www.globalpublishers.info

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s