Rais Andry Rajoelina katika ziara ya kikazi nchini Tanzania

 

ra1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mhe Andry Rajoelina wakati wa  mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam jana Mei 3, 2013. 

PICHA NA IKULU

ra2

Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam jana jioni  , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 

Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi hao wanatarajiwa kufanya  mazungumzo baadaye leo Ikulu, Dar Es salaam.

Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari  mwaka huu.

Rais Kikwete alipokutana mara ya mwsho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi  Rais wa zamani wa Madagascar Mhe Marc Ravalomanana  asigombee katika uchaguzi  mkuu huo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

03 Mei, 2013

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s