Watu 74 wapoteza maisha katika mafuriko nchini Kenya

 

 

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limetangaza kuwa, kwa akali watu 74 wamepoteza maisha na wengine karibu ya laki moja hawana makazi baada ya kunyesha mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo kadhaa nchini humo. 
 
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limetangaza kuwa, watu 40 wamefariki dunia katika eneo la Rift Valley, 21 mashariki mwa Kenya na wengine 7 katika eneo la Pwani. 
 
Shirika hilo limesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mmomonyoko wa udongo katika eneo la Nandi lililoko Rift Valley. 
 
Shirika hilo limewataka wakazi wa eneo hilo kuhamia sehemu nyingine yenye usalama zaidi. Mafuriko hayo yameleta maafa makubwa ya kifedha na miundombinu na kukwamisha shughuli muhimu za sekta za kilimo na elimu katika maeneo hayo.

Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada ya kibinadamu yameeleza kuwa zinahitajika zaidi ya dola milioni tatu, laki saba na elfu themanini kwa shabaha ya kusaidia maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo.Chanzo:swahilivillablog

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s