VITUKO VYA KWENYE GAME: LINAH NA BARNABA WASUSIA KIAINA SHOW YA MIAKA 13 YA LADY JAY DEE

 

 

 

 

hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye malipo. Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo. 

“Dada yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema Linah. “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.”

Kwa upande wake Barnaba amesema hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao kama wasanii wana menejementi na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka ulishindwa kufikiwa na pia walikuwa na booking zingine.

Hata hivyo Barnaba amesema hakuna ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee. “Tuko safi tu na dada, mbona tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye maongezi mazuri tu, tulishaongea na hili suala liko vizuri.” Amesema Barnaba
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s