MBIO ZA MBUZI ZA HISANI ZA DAR ES SALAAM 2013 ZAKARIBIA!

Mbuzi wakichuana ili kumpata mshindi katika mashindano ya mbio za mbuzi za hisani za mwaka jana. (Picha ya Maktaba)

‘Mbuzi Mmoja tu, Anaweza Kuleta Mabadiliko’     
Waandaji wa mbio hizo maarufu nchini wamesema jijini hapa leo kuwa kwa sasa mbuzi watakaoshiriki mbio hizo wako kwenye kambi za mazoezi huku zawadi kemkem za kuvutia zikiwa zimeandaliwa kwa mwaka huu.

“Tunachokihitaji kwa sasa ni uwepo wa mashabiki watakaohudhuria tukio hilo la kufurahisha na hivyo kutusaidia kufikia lengo tulilojiwekea la kusanya shilingi bilioni moja kwa ajili ya taasisi mbalimbali za kujitolea nchini,” Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Mama  Karen Stanley alisema.

“Siku hiyo tumeandaa sehemu mahsusi kwa ajili ya aina mbalimbali ya vyakula vya kuvutia kutoka sehemu maarufu zinazohusika na mapishi jijini Dar kama Rose Garden, Arca di Noe, Black Tomato na Q Bar.

“Pia tutakuwa na eneo lililokarabatiwa kwa ajili ya michezo ya watoto litakalowafanya watoto watakaofika kufurahi na kuikumbuka siku hiyo. Lipo eneo jingine jipya kwa watoto wadogo zaidi huku eneo jingine lililotayarishwa na Neverland Playgroup and entertainment kwa ajili ya watoto wakubwa zaidi litakalokuwa na michezo kama sarakasi, ngoma, kucheza muziki na wachekeshaji kutoka asasi ya  Kigamboni Community Centre.”

Tukio hilo ka kifamilia la kila mwaka litafanyika Juni Mosi mwaka huu kwenye eneo la Green, mtaa wa Kenyatta kuanzia saa sita mchana hadi saa 11.30 jioni. Gharama za tiketi ni Sh 5,000 kwa watu wote na zitauzwa getini.

Mbio hizo za mbuzi za hisani zinafanyika kwa mara ya 13 mwaka huu. Tangu yalipoanzishwa mwaka 2001, tayari zaidi ya shilingi milioni 660 zimekwisha kusanywa kwa ajili ya mashirika na taasisi mbalimbali za kujitolea nchini. 

Mwaka jana tukio hilo liliweka rekodi kwa kukusanya shilingi milioni 115 kwa kwa ajili ya mashirika 15, huku wahudhuriaji wakifika 4,200 na kulipa kiingilio getini.

Mama Stanley alisema: “Mwaka huu tunatarajia kufanya makubwa zaidi. Tunafuraha ya kuwa na wadhamini wengi muhimu sana, ambao ndio uti wa mgongo wa tukio lenyewe. Bila wao hakika tusingekuwa hapa. Kwa namna ya pekee yunatoa shukrani kwa wadhamini wa mbio hizo Southern Sun, Coca-Cola, Tanzanian Breweries Limited, Mantra Tanzania, Erolink, FNB na Symbion.

“Lakini ukweli ni kwamba bila ujio wa watu wa kawaida, mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za Dar, wenyeji na wageni, kushuhudia mbio hizo za aina yake kusingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo karibuni nyote, msiisahau siku hiyo ya ajabu kabisa!”

Miongoni mwa zawadi kubwa kwa mwaka huu ni tiketi ya kwenda Ulaya na kurudi itakayotolewa na SWISS, safari ya kwenda kwenye mbuga ya wanyama ya Selous na kifurushi cha kupata mtandao wa Intaneti  kwa mwaka mzima kutoka UhuruOne kikiambatana na vifaa na uunganishaji.

Dhana ya mwaka huu, ‘Viumbe wa Baharini na Mabaharia’, inaweza kuvutia wengi wanaopenda kuingia kwenye mashindano ya mavazi ya kuvutia huku kukiwa na zawadi nono kwa kundi litakalovaa vyema. Kutakuwa pia na shindano la mavazi maalumu kwa watoto na zawadi kwao.

Mama Stanley alisema: “Ukija umevaa kwa mtindo wa nguva au baharia, au hata ukiwa kawaida tu utafurahia mambo tuliyokuandalia mwaka huu.”

Kwa habari zaidi tembelea tofutti yetu; www.goatraces.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s