Vipodozi vyenye kemikali, dawa bandia zinavyowaua Watanzania

 

Baadhi nya madhara ya utumiaji wa vipodozi vyeme kemikali 

 

Na Florence Majani, Mwananchi  (email the author)
Kwa ufupi

Utafiti wa Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Georgia, Atlanta, Marekani, Kelly Lewis wa kitengo cha Sosholojia, kuhusu wanawake wanaotumia ‘mkorogo’ Tanzania umebainisha hayo.

 

Pen V hutumika kutibu maradhi ya kuambukiza, vidonda. (Antibiotic) Wakaguzi walipoikagua waligundua kuwa dawa hiyo inaganda ndani ya kopo pindi unapoliinamisha.

 

Bidhaa zinazosadikiwa kukuza maumbile(hip lift up na hip massage cream), nazo zilipigwa marufuku ingawa bado zinauzwa kwa njia ya panya katika maduka.

 

Mkurugenzi huyo wa TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini anasema kuwa thamani ya dawa, chakula na vipodozi vilivyoteketezwa na mamlaka yake kwa mwaka 2010/2011 ni Sh844. 3 bilioni.

 

Madhara
Sonda anasema kuwa matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu kwa kaisi kikubwa husababisha maradhi ya figo, fangasi, saratani ya ngozi, ini na mzio.
Mfamasia katika Hospitali ya Amana, Christopher Masika anasema kuwa Serikali pamoja na wadau wengine wa afya hawana budi kuwafundisha Watanzania namna ya kubaini dawa bandia.

 

Anasema kwamba matumizi ya dawa bandia yana madhara mengi. “Kwa mfano Flagyl haitibu malaria bali inatibu vimelea vya maradhi ya tumbo, mtu akinywa kwa lengo la kutibu malaria atakuwa hajatibiwa na ugonjwa wake utakuwa palepale na baada ya siku chache malaria inaweza kujirudia,” anasema.

 

Anasema kuwa ndiyo maana siku hizi dawa za malaria zinakuwa sugu na watu wanaendelea kuugua ugonjwa huo kutokana na ujanja mbaya unaofanyika.Kuhusu vipodozi vyenye viambata sumu, Famasia Masika alisema kuwa vipodozi vyenye madini ya Zebaki au Mercury husababisha maradhi ya saratani.

 

“Kwa mfano hydroquinoline, hiki ni kiambata sumu ambacho kinaharibu ngozi, ni rahisi kupata maambukizi ya ngozi kwa sababu ngozi ya mtumiaji inakuwa nyepesi mno.

 

Mtu huyo si rahisi kupona hata akijeruhiwa,” anasema
Anasema ngozi ya binadamu ina kinga iitwayo ‘therapine’ ambayo hupukutishwa mtu anapotumia vipodozi vyenye viambata sumu.
Hivyo ni rahisi kupata saratani kwa kuwa kinga hiyo huondolewa.

 

“Lakini pia matundu ya kutolea uchafu yanazibwa, hivyo mwili hautoi uchafu na sumu inabaki mwilini,” anasema Mfamasia Masika
Anasema kuwa mwanamke anayetumia vipodozi hivyo, ngozi yake huwa laini mno na chochote kitakachoingia huiathiri.

 

Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza anasema kuwa mamlaka hiyo imepiga marufuku vipodozi vyote vyenye viambata sumu, ingawa bado watu wanavitumia.“Madhara yake ni makubwa, mwanamke mjamzito ni rahisi kuzaa mtoto taahira, au mimba ikatoka,” anasema Simwanza.

 

Daktari wa Magonjwa ya Ngozi wa Kituo cha Afya Centre, Isaack Maro, anasema wanawake wanaotumia vipodozi vyenye viambata sumu huathirika kwa kiasi kikubwa bila kujijua.Anasema madini ya zebaki yanayotumika katika vipodozi vingi hayatoki kwa urahisi mwilini.

 

Dk Maro anasema madini hayo hujazana mwilini kwa muda mrefu na kusababisha maradhi.Chanzo:Gazeti la Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s