LOWASSA, MAGUFULI NGOMA NZITO

 

 

Na Mwandishi Wetu
WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, gazeti hili limefanya utafiti wa watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo na lina matokeo ambayo yanaonesha ngoma nzito.

 

Edward Lowassa.

Utafiti huo ulioendesha kwa njia ya kura za maoni kwa wasomaji wa gazeti hili kwa wiki 14 umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli wangekabana koo kwani matokeo yameonesha kutofautiana kidogo kwa kura.
Lowassa anayewakilisha Jimbo la Monduli ameongoza katika orodha hiyo kwa  kupata kura 759,611 ambazo ni asilimia 34 na Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato amepata kura  692,587 ambazo ni asilimia 31.

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Bernard Membe amepata kura 235,757 ambazo ni asilimia 11 na amekaribiana na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki Samwel Sitta aliyepata kura 201,074 ambazo ni asilimia 9, kukiwa na tofauti ya asilimia mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Bernard Membe.

Wengine waliopigiwa kura na kura zao katika mabano ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (178,732, asilimia nane), Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi za Afrika, Dk. Salim Ahmed Salim (89,366 asilimia nne) na Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Asharose Migiro (44,683 asilimia mbili).

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki Samwel Sitta.

Kura zilizoharibika ni asilimia moja kwani wapo waliokuwa wakichagua zaidi ya jina moja katika sms moja na wengine kuandika majina ya watu ambao hawakuwemo katika orodha ya wapigiwa kura.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wameshauri kwamba gazeti hili lifanye utafiti mwingine kwa kumpambanisha mgombea huyo wa CCM aliyeshinda na wapinzani.

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

Awali wasomaji wetu walichagua wanasiasa mbalimbali kutoka CCM ambao wanafaa kuwa viongozi wa nchi na uongozi wa gazeti hili ukateua wanane waliotajwa mara nyingi na wananchi kisha kuwapambanisha.Chanzo:www.globalpublishers.info

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s