MWENYEKITI WA BARAZA LA MITIHANI – (NECTA ) ANADAI KUWA HAYUKO TAYARI KUYABADILI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE -2012

 

 

 

 

Kuna  tetesi  kwamba  Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amegomai kubadili matokeo ya Kidato cha Nne- 2012.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka ‘kuboreshwa’ kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa.

 

 

 

 “Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?” alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo. 

 

 

 

Hata  hivyo, siku  za  hivi  karibuni  mwanahabari  wetu  alizungumza  na  Ofisa Habari wa NECTA, John Nchimbi ambaye alisema wamekwishapokea maelekezo kwa barua na kufanyia kazi ili kujitahidi ndani ya muda mfupi matokeo yawe yametoka.

 

 

 

Nchimbi alikiri kuwapo kwa kasoro katika matumizi ya mfumo huo mpya wa usahihishaji, kwani hawakushirikisha wadau wengi kabla ya kuanza kutumia, lakini lengo la Baraza lilikuwa jema katika kukuza elimu nchini

 

 

“Kutokana na tangazo hili, wanafunzi hawa wote hawana matokeo tangu juzi ( yalipofutwa bungeni ), hivyo wasubiri matokeo mapya yatakayotangazwa, na waelewe wazi kuwa si lazima waliofeli wafaulu wote,” alisema  Nchimbi.


Advertisements

3 Comments

  1. mimi nafikiri serikali hawajui wanafanya nini.maana mpaka sasa wazazi wameshafanya njia mmbadala juu ya watoto wao, leo serikali inasema inabadilisha matokoe ili yaweje?

    Like

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s