Lady Jay Dee kuripoti Mahakama ya Kinondoni kesho

 

 

 

jd 36b09

Na Andrew Chale
MWANAMUZIKI nguli wa bongo na kiongozi wa yenye mvuto nchini bendi ya ‘Machozi’, Judith Wambura ( Lady JayDee) au Jide ama #Teamaanaconda#, anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni siku ya Jumatatu Mei 13, kufuatia kufikishiwa kwa taarifa hizo Gadna G Habash ‘Captain’ ambaye ni Meneja na mume wa Lady Jay Dee. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mchana wa leo, Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa kwa Lady Jay Dee kufika Mahakama ya Kinondoni, siku ya Jumatatu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni, Hii ni kufuatia kwa jana kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo na walikuja na barua ya kumkabidhi Lady Jay Dee mwenyewe hata hivyo hawakumkuta” alisema Gadna.
Aliendelea kueleza kuwa, hata alipowaeleza watu hao wamkabidhi yeye hiyo barua watu hao walisema ilikuwa si lahisi zaidi alitakiwa akabidhiwe mlengwa, hivyo kumueleza kuwa wito wa kufika mahakamani siku ya Jumatatu, na aliwakubalia kwa hilo.
Hata hivyo, Gadna alisema hajajua Lady Jay Dee anaitiwa nini na kwa sababu ya nani zaidi amemwelezea na amesema watatekeleza wito huo wa kufika Jumatatu Mahakamani hapo.
Aidha, kupitia kwenye ukurasa wake wa Kijamii wa facebook, Lady Jay Dee aliandika: “Ratiba ya Usiku wa leo, ni Machozi Band, kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea…” aliandika Jide kwenye ukurasa huo ambao mpaka hatua ya mwindishi anatembelea ‘post’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ambayo watu mbalimbali walipata kuchangia.
Maoni hayo yanayokaribia zaidi ya 558 na, ‘Like’ zaidi ya 756 na ‘Share’ zaidi ya 20, ambapo wengi wao wameweza kumuhusisha moja kwa moja na Mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba kuwa ndie aliyefanya hivyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali na moja ya gazeti hivi karibuni ilimnukuu Ruge kuwa amejiandaa kuchukua hatua ikiwemo ya kisheria dhidi ya Lady Jay Dee baada ya kumsema kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s