MATOKEO MABOVU YA KIDATO CHA NNE YATACHELEWESHA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA

 

 Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi  huu yatachelewa  ili kutoa nafasi kwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),  kurekebisha matokeo mabaya ya mitihani  kidato cha nne ya mwaka jana yaliyofutwa na serikali  mwezi huu.
 
Matokeo ya kidato cha sita ambayo huwa yanatangazwa mwanzoni  mwa mwezi Mei mpaka sasa hayajatolewa  na kwamba hayatatangazwa mpaka matokeo mapya ya kidato cha nne yatakaporekebishwa rasmi.

Alipoulizwa  juu ya suala hilo, Naibu Waziri   wa Elimu na  Mfunzo ya Ufundi  Philipo Mulugo alisema ingawa wakati huu ndio unaopaswa yatangazwe matokeo ya kidato cha sita haitafanyika hivyo hadi yatangazwe matokeo mapya ya kidato cha nne baada ya kufutwa.


Hata hivyo, akasema huenda yakatolewa  pamoja au yakafuata wakati mwingine lakini mara baada ya  kukamilisha kazi ya kurejea na kusahihisha matokeo ya kidato cha nne.


“Siyo kwamba yamechelewa kwani muda wa kujiunga na chuo ni Septemba hivyo haitawaathiri kwa hilo,” alisema Mulugo.


Kuhusu hatma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambao wapo mashuleni wanaendelea na masomo ya kidato cha sita, alisema  kama kutakuwa na wanafunzi ambao wapo madarasani  shule zilizowasajili  zitakuwa hazijafuata mfumo wa elimu unavyoelekeza.

Alifafanua kuwa mfumo wa elimu kwa kidato cha nne ulibadilishwa na kwamba endapo mwanafunzi akifaulu anatakiwa kujiunga rasmi kidato cha sita  Julai na si vinginevyo.

Alisema licha ya  ucheleweshaji  wa matokeo  hali hiyo haikuwaathiri wanafunzi hao kwa kuwa ratiba ya kwenda masomoni  haijaanza kwa mujibu wa kalenda  ya shule ya serikali.


Serikali ilifuta matokeo ya kidato cha nne ya 2012 na kuiagiza Necta kuyaandaa upya kwa kutumia utaratibu wa usahihishaji na upangaji madaraja uliotumiwa mwaka  2011

Taarifa ilisema mfumo uliotumika  mwaka jana na kusababisha wanafunzi kushindwa vibaya haukufanyiwa utafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika. 

Matokeo hayo  yaliyotangazwa  mwezi  Februari mwaka huu yalionyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi walishindwa mtihani.
Advertisements

3 Comments

 1. Baraza la mtihani Tanzania linatakiwa kuwa wazi kwa wanafunzi kuhusu mabadiliko yanayotolewa na baraza la mtihani.Kwani hali hiyo inatupa wasiwasi juu ya matokeo ya kidato cha sita nayo yaweza kuwa mabaya kama ya kidato cha nne 2012

  Like

  Reply

 2. Niko ladhi kusema hivi! Si waziri wala naibu waziri wote ni wapuuzi! wanawezaje kuwa na maamuzi yasiyokuwa na busara kama haya? mbona mnakurupuka tu? kwani hilo hamkuliona mwanzo? kwa nn mtangaze matokeo then mnasubiri nini mtasikia kutoka kwa watanzania waliochoshwa na mambo yenu watasemaje ili tume iundwe,watoto wajiue harafu mrekebishe matokeo? sasa mnafufua na wale waliojiua?

  Like

  Reply

 3. matokeo ya kidato cha nne moja ya kikwazo pia ni pamoja na mda mdogo wanaopewa na wasimamizi wao,msimamizi akiona amechoka tu basia atarusha mda mbele au atajipangia mda wa kusema pens down simama juu….ni hilo tu

  Like

  Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s