Nchi ya Afrika Kusini yalaani uingiliaji wa Wamagharibi Syria

 

 

 

Bi.Phumla Williams Msemaji wa serikali ya
 Afrika Kusini

 

Serikali ya Afrika Kusini imeitaka jamii ya kimataifa kuheshimu haki ya kujitawala ya Syria, sanjari na kujiepusha na uingiliaji katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.

 

 

 

Phumla Williams Msemaji wa serikali ya Afrika Kusini ameongeza kuwa, wenyewe wananchi wa Syria wanapaswa kuutatua mgogoro wa nchi hiyo bila ya uingiliaji wa madola ya kigeni.

 

 

 

Wiki iliyopita, serikali ya Afrika Kusini ililaani vikali hatua ya ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia ardhi ya Syria na kutahadharisha kuwa, hatua hiyo itazidisha kuvuruga amani na uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati.

 

 

 

Aidha serikali ya Pretoria imetaka ukomeshwe mpango wa baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu wa kuyapelekea silaha makundi ya kigaidi nchini humo.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s