FLORA BAHATI LYMO NI MWANAMKE ANAYEDAI KUBAKWA NA MBUNGE WA CHADEMA

BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda kuwa amembaka
 

Katika uchunguzi wake, hivi karibuni ,Uwazi lilielezwa kuwa kuna habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.

 

 

 

 

 

Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo uwazi likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
 

 

 

 

“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).

 

 

 


Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
 

 

“Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya chama chake  nikakataa, ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa kwenye mkutano huo na balozi na rais kwa ajili ya ushushushu.


“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu, mbunge huyo na wenzake nao walitoka. 

 

 

 

 

 

Tukiwa njiani wenzake walikwenda kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu, nilimkubalia. 

 

 

 

 

 

Alipofika ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa umeniponza.


Alinirukia, akaniburuza hadi kitandani kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki ndipo akanivamia maungoni, akanichania nguo zangu akitaka nimwachie atimize lengo lake la kuniingilia kimwili kwa nguvu.
 

 

 

 

“Nilijitahidi ili asifanikiwe, nikamwambia amekwisha kwani lazima nimwanike ndipo akanipiga nusu aniue akisisitiza kuwa kama nitauanika uovu wake huo au kuchukua hatua zozote ataniua.
 

 

 

 

“Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu atishie kuniua, unyama gani huu?”
Flora anaendelea kusema:
“Katika purukushani hiyo, nilipopata mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya polisi 999 kuomba msaada. Alipoona hivyo alitoka na kutokomea kusikojulikana. Polisi walipofika hawakufanikiwa kumkamata.”

Flora alisema polisi walimchukua na kila kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake hadi kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti, wakampa namba ya jalada la kesi inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo mbunge huyo anasakwa na Polisi wa London, akikanyaga tu Uingereza lazima akamatwe akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia kuua.
 

 

 

 

Flora akaongeza: “Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu alikuwa na passport za kidiplomasia ambazo nyingine hakutumia jina lake halisi.

 

 

 

“Kesho yake nilisikia alikimbilia Ujerumani, nikawaambia polisi lakini walikumbana na tatizo lile kwani majina niliyowapa siyo aliyotumia kuingia Ulaya.
 

 

“Januari mwaka huu nilipotaka kurudi nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya hapa (Uingereza) ilinipa barua ambayo nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi nikafunguliwa faili Namba Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini ya R.C.O Ramadhan Ng’anza.

 

 

“Niliwaeleza kuwa mtu anayetaka kuniua ni mbunge huyo. Kweli waliahidi kunisaidia, nilipoondoka kurudi London niliwasiliana na polisi Kilimanjaro lakini niliona kama kuna kitu au mbunge huyo yupo juu ya sheria kwani walikana kunifahamu.
“Sitachoka kutafuta haki na kutetea wanawake wanaobakwa kila siku wanaona aibu kusema, naamini aibu haipo kwa mbakwaji bali kwa mbakaji, yule …. (anataka jina) ni mbakaji.
 

“Nimesharipoti mashirika mengi ya haki za binadamu ya Uingereza. Kuna siku nilishinda mahakamani, kule ni yeye tu anasubiriwa atiwe mbaroni akasimame kizimbani ndipo dunia itajua ninachokisema.”


Flora allisema kama kweli mbunge huyo ni mwanaume aende tena jijini London kama hatasimamishwa kizimbani na kuozea jela.”
 

Chanzo: Gazeti la uwazi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s