BUNGENI :SERIKALI KUENDELEA NA MPANGO WA KUJENGA BOMBA LA GESI KUTOKA MTWARA-LINDI MPAKA DAR ES SALAAM

 

 

IMG_1979Na Lydia Churi, MAELEZO-DODOMA

 

Serikali itaendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi asilia kutoka mkoani Mtwara, Lindi hadi Dar es Salaam. Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ameliambia bunge leo mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya mwaka wa fedha 2013/2014.

 

Alisema mradi wa kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam utahusisha  ujenzi wa bomba  lenye urefu wa kilometa 532 ambapo bomba hilo litakuwa na uwezo wa kusafirirsha futi za ujazo za gesi asilia milioni 784 kwa siku.

 

 

Alisema mradi huo utaigharimu Serikali shilingi bilioni 1,960 ambapo kazi za usanifu wa mradi na ulipaji wa fidia kwa wananchi wapatao 3,092 waliopisha maeneo ya mradi zimekamilika. Hatua za awali za ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi asilia zimeanza.

 

 

Waziri Muhongo alisema kutokana na mradi wa gesi asilia wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara watapata manufaa mbalimbali yatokanayo na mradi huo ikiwa ni pamoja na tozo ya asilimia 0.3 ya mauzo ya gesi asilia, huduma za jamii kama vile zahanati, shule, umeme, maji  na mafunzo katika vyuo vya ufundi (VETA) na sekondari.

 

 

Wakati huo huo, Serikali imefanikiwa kukamata madini yenye thamani ya shilingi bilioni 13.12 kati ya mwezi Oktoba 2012 na April 2013 yaliyokuwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume na sheria.

 

 

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ameliambia bunge leo mjini Dodoma kuwa wahusika wameshachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010.

 

 

Alisema katika kuimarisha usimamizi wa biashara ya madini nchini, Serikali kupitia wakala wa madini (TMAA) imeanzisha madawati maalum ya kukagua madini yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia viwanja vya ndege vya kimataifa vya Dar es salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

 

 

 Wizara ya Nishati na Madini imeomba kuidhinishiwa na Bunge zaidi ya shilingi trilioni moja ambapo asilimia 90 ya fedha hizo ni kwa ajili ya maendeleo na asilimia 10 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Aidha Fedha za ndani ni asilimia 56.27 na za nje ni asilimia 43.73.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s