Machafuko Mtwara,Ofisi ya CCM yachomwa moto

 

 

 

MAPAMBANO kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara umefika katika hatua mbaya,kiasi cha mtu mmoja kudaiwa kujeruhiwa vibaya baada ya kurushiwa bomu wakati wa mashambulizi hayo katika eneo la Magomeni.

 

 

 

clip_image001

 

Mbali na kujeruhiwa kwa mtu huyo aliyekuwa katika maandamano ya kupinga Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia imechomwa moto.

 

 

 

Taarifa zilizonaswa na Fahari ya Kusini hivi punde zinadai kwamba wananchi wa Mkoa wa Mtwara wamefungiwa majumbani tangu asubuhi, huku Jeshi la Polisi likifanya msako wa nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwanasa watuhumiwa wanaodaiwa kuchochea maandamano hayo kwa njia ya vipeperushi.

 

 

 

Shuhuda wa wa tukio hilo ameitaarifu Fahari ya kusini kwamba waandamanaji hao wameapa kufa endepo serikali itaendelea na mipango yake ya kusafirisha gesi hiyo hadi Jijini Dar es Salaam. 

 

 

 

 

“Hali hapa ni mbaya, tangu asubuhi wananchi wote wamefungiwa ndani ya majumba yao, hakuna anayeruhusiwa kutoka nje, Polisi wanapiga mabomu ya machozi kila mtaa huku wakiwasaka watuhumiwa waliosambaza vipeperushi na kuwatawanya wandamanaji waliozagaa katika mitaa mbalimbali, mpaka hivi sasa kuna mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mashambulizi ya raia na Asakari Polisi wanaotumia mabomu ya machozi na silaha zigine za moto”alisema shuhuda wa tukio hilo.

 

 

 

 

Hata hivyo imedaiwa kuwa hali hiyo imesababisha barabara zote kufungwa kiasi cha kuzuia mabasi yanayoingia na kutoka katika mji huo toka asubuhi, kuna baadhi ya mitaa matairi yamechomwa moto barabarani, magari ya FFU yametanda kila kona za mji, huku taarifa zidi ikifafanua kwamba hakuna mawasiliano, milio ya mabomu inasikika kila kona na hali ya utulivu sio ya kuridhisha, Askari wa zima moto wamesambaa kuzima moto na kuna baadhi ya nyumba maeneno ya Shangani zimechoma moto. 

 

 

 

Nyumba ya mwandishi wa Habari wa TBC kassim Mikongoro inasemekana Imechomwa moto mchana huu. Hali ni tete Askari wawili na raia mmoja wanasadikika kuuawa.

 

 

 

Breaking News: Makinda ahairisha Bunge.

 

 

 

Spika wa Bunge Anna Makinda ameahirisha Kikao cha Bunge mpaka kesho serikali itakapotoa taarifa kamili kuhusiana na vurugu zinazoendelea huko Mtwara.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s