Dawa ya Kitaalam ya kufukuza Panya kwa Kutumia haja ndogo yatafitiwa.

 

rat01

Na Hassan Silayo- MAELEZO

Kituo cha utunzaji wadudu (Pest Management Centre) kinafanya utafiti wa kutumia harufu ya haja ndogo ya paka kufukuza panya waharibifu.

Hayo yamesemwa jana na Mtafiti wa kituo hicho kilichoko chini ya chuo kikuu cha kilimo cha sokoine (SUA) Profesa Christophar Sabuni katika maonesho ya Taasisi za Elimu ya Juu jijini Dar es salaam.

Profesa Sabuni alisema kuwa utafiti huo utasaidia wananchi kupata njia mbadala na salama kwa binadamu ya kufukuza panya sehemu mbalimbali kama kwenye mashamba na majumba, badala ya kutumia sumu kama inavyofanyika sasa.

“Utafiti huu unalenga kumsaidia mwananchi kufukuza panya na kuondoa uharibifu hasa tukilenga kwenye mazao na hata majumbani kwa maana ndio wanaopata adha kubwa ya wanyama hawa, utafiti huu utawasaidia sana” alisema Profesa Sabuni.

Pia alifafanua mchakato wa tafiti hii ulianza kwa kuangalia ni haja ndogo ya paka wa jinsia gani unaoweza kupata dawa ya kufukuza panya na kugundua kuwa paka wa kike ndio bora zaidi.

“Utafiti wowote unaoufanya huna budi kuangalia njia itakayosaidia kutimiza lengo haraka, ndipo tukaamua kuangalia jinsia stahiki kati na dume na jike na tukagundua kuwa harufu ya mkojo wa paka jike itatufaa zaidi” alisema Profesa Sabuni.

Alisema haja ndogo hiyo wanaichakata kutoka kimiminika na kuwa katika hali ya ungaunga ili kurahisisha utumiaji wa dawa hiyo.

Alifafanua kuwa utafiti huo utakaochukua takribani miaka mitano ni mwendelezo wa tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa na kituo hicho, ambapo awali ilihusisha utafiti wa mafunzo ya panya kwa ajili ya kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi. 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: