MISS GEITA 2013 KUFANYIKA JUNI MOSI MWAKA HUU

Baadhi ya warembo waliokutwa katika mazoezi ya kushiriki taji la Miss Geita 2013.

Na Salum Maige, Geita
24. 05. 2013
KINYANG’ANYIRO cha kumsaka mrembo wa kwanza wa mkoa wa Geita  “Miss Geita 2013’’ kimeanza huku warembo 16 kutoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya za mkoa huo wakiwa wamejitokeza kushiriki mashindano hayo.
Mwandaaji wa mashindano hayo, Miriam Gabriel, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya RedRose and General Supply amesema maadalizi ya shindano hilo yanaenda vizuri kutokana na mwitikio wa wadau wa mashindano hayo na kwamba uzinduzi wake utafanyika Jumamosi ya wiki hii na viongozi mbalimbali wa serikali, wafanyabiashara na wakulima watashiriki katika uzinduzi huo.
Alisema warembo hao wapo kambini katika Hoteli ya Katoma Hill  mjini Geita tangu Mei 20, mwaka huu wakifanya mazoezi ya kuwania Taji la Miss Geita mwaka 2013 ambaye atashiriki mashindano ya kumtafuta Miss Kanda ya Ziwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mirian Gabriel ni kwamba shindano hilo linatarajia kufanyika juni Mosi, mwaka huu katika ukumbi wa Disire na mgeni Rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Geita Said Magalula huku wasanii mbalimbali wa Muziki wakiwemo Bob Haiza na Binti Madaha wakitumbuiza shindano hilo.
Alisema shindano hilo linadhaminiwa na Benki ya CRDB, Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Katoma Hill Hotel, Disire Pup na Gambo Hotel

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s