Viongozi wa nchi wanachama wa AU kujadili changamoto zinazolikabili bara la Afrika

 

 
Na Flora Martin Mwano
 
Maadhimisho ya miaka hamsini ya Umoja wa Afrika AU yameendelea mjini Addis Ababa Ethiopia ambapo viongozi toka nchi wanachama wanashiriki katika mkutano wa umoja huo unaojadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Afrika.
 
Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika AU, Nkosazana Dlamini-Zuma
 
Akifungua sherehe hizo siku ya jumamosi Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn aliwataka viongozi wa Afrika kuimarisha umoja huo kwa kupiga vita umasikini na migogoro inayoendelea kushuhudiwa katika baadhi ya nchi wanachama.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa AU Nkosazana Dlamini-Zuma amesisitiza kuwa migogoro inayolikabili bara hili itakomeshwa kwa mshikamano na umoja utakaoonyeshwa na wahusika.
 
Viongozi mashuhuri waliohudhuria sherehe hizo toka nje ya bara hili ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki-moon, Rais wa Ufaransa Francois Hollande, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, Naibu wa Waziri Mkuu wa China Wang Yang na Rais wa Brazili Dilma Rousseff.
 
Sherehe hizo pia zilishuhudia serikali ya Brazili ikiweka wazi mpango wa kutajka kusamehe madeni ya jumla ya dola za Marekani milioni mia tisa katika nchi kumi na mbili za Afrika, miongoni mwa nchi zitakazonufaika na msamaha ni Tanzania, Congo-Brazzaville na Zambia.
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s