MIDUME YAGOMBEA KUMUOA WASTARA!

Na Imelda Mtema

TAKRIBAN  wiki moja baada ya kumaliza eda tangu alipofariki mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari 2, mwaka huu, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma anagombewa na midume ikitaka kumuoa.

Wastara Juma.

Akizungumza na ‘The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda akiwa nchini Oman, Wastara alifunguka kuwa tangu amalize eda yake hiyo amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.

“Jamani mpaka nahisi kuchanganyikiwa kabisa, wanaume zaidi ya mia tano hata…

 

 


Na Gladness Mallya
TUMUOMBEENI! staa wa Injili na filamu za Kibongo, Sara Mvungi ni mgonjwa anayesumbuliwa na vidonda vya tumbo na malaria ambavyo vimemfanya alazwe akiwa hoi.
Akizungumza na The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda kwa taabu wikiendi iliyopita kwenye Hospitali ya TMJ Mikocheni, jijini Dar alikokuwa amelazwa, Sarah alisema alianza kuugua siku tatu kabla ambapo alikuwa akitumia dozi ya malaria.
Alisema kuwa wakati akiwa kwenye dozi hiyo, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya kupata homa kali ambapo alikimbizwa hospitalini hapo huku maradhi ya vidonda vya tumbo ya muda mrefu nayo yakimsumbua.
Akiwa hospitalini hapo, Ijumaa Wikienda lilimshuhudia Sara akiwa na ‘dripu’ ikimiminika kwa kasi kuingia mwilini ambapo alikiri kuwa mwanzoni alikuwa na hali mbaya lakini walau kwa sasa anaendelea vizuri.
“Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri, nilikuwa siwezi kutembea hadi nishikwe mkono, vidonda vya tumbo vinaniuma sana na homa nayo inanisumbua kwa siku tatu sijaweza kufanya kazini,” alisema Sarah ambaye pia ni nesi.Chanzo:www.globalpublishers.info

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s