MSIMU WA NANE WA SHINDANO LA BIG BROTHER AFRICA WAZINDULIWA LEO, MAMBO YANOGA UKUMBI WA SAMAKI SAMAKI CITY CENTRE JIJINI DAR ES SALAAM!!

 

 

Uzinduzi wa shindano la Big Brother Africa umefanyika usiku huu katika ukumbi wa Samaki Samaki City Centre maeneo ya Posta jijini Dar es salaam ambapo wawakilishi wa tamasha hilo kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wamewekwa hadharani.

 

Uzinduzi huo umeoneshwa moja kwa moja na rununga ya DSTV huku Bi.Feza Kessiy na Ammy Nando wakitajwa kuwakilisha Tanzania katika msimu wa nane wa Big Brother Africa.

 

Kwa hapa Tanzania uzinduzi huo ulidhaminiwa na kampuni ya simu za mkonono ya Airtel ambapo wametoa zawadi mbalimbali zilizoshindaniwa na watu waliohudhuria katika zoezi hilo.

 

Burudani kubwa ya muziki ilitawala katika ukumbi huo ambapo wageni waalikwa wamefurahi pamoja kwa kula na kunywa.

 

SONY DSCKutoka kushoto ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania,  Furaha Samalu, (katikati) meneja rasilimali watu wa Multi Choice Tike Mwakitwange,  wa kwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Multi Choice  Barbara Kambogi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Uzinduzi wa Big Brother Africa katika ukumbi wa Samaki Samaki City Centre maeneo ya Posta jijini Dar es salaam usiku wa leo SONY DSCMhudumua wa kampuni ya simu ya Airtel ambao ni wadhamini wa Uzinduzi wa Big Brother Africa mwaka huu (mwenye T-shirt nyekundu) akiwahudumia wateja wanaotaka kusajili namba zao pamoja na kujiunga na huduma ya Airtel Money wakati wa tamasha hilo SONY DSCMeneja uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kulia) akizungumza na wageni waalikwa , waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Big Brother Africa , pamoja na huduma za MultiChoice kwa wateja wake SONY DSCBalozi wa Airtel Tanzania, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya AY akikabidhi kadi ya mwaliko mara baada ya kuingia katika ukumbi wa Samaki Samaki City Centre SONY DSCWasanii kutoka Afrika kusini wakiburudisha watu katika runinga ya DSTV wakati wa uzinduzi wa Big Brother Africa leo katika ukumbi wa Samaki Samaki City Centre maeneo ya Posta jijini Dar es salaamSONY DSCWadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huoSONY DSCWadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatilia matangazo ya kituo cha televisheni cha DSTV kinachoonesha matangazo hayo moja kwa moja  SONY DSCMshindi wa zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy, bwana Dennis Fussi kutoka Magazeti ya Daily News na Habari Leo.  Zawadi hiyo imetolewa usiku huu kutoka kampuni ya simu za mkonono inayoongoza kutoa huduma bora ya Airtel katika Ukumbi wa Samaki Samaki City Centre maeneo ya Posta jijini Dar es salaam

 

Chanzo: Fullshangweblog
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s