Waunda timu ya urais Uchaguzi Mkuu wa 2015

 

 

 

Mwanza. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema wakati ukifika, yeye na rafiki zake Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, watachagua mmoja wao watakayeona anafaa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
 
Samweli sitta
 
Waziri Sitta aliyasema hayo jana katika Kongamamo la Mawasiliano katika Nyanja za Digitali la wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT), Mwanza.
 
Mara ya kwanza, Sitta aliwataja rafiki zake hao juzi wakati wa harambee ya kuchangia Kanisa Katoliki, Josephine Bakita, Parokia ya Igoma, Mwanza.
 
Pia alisema hatagombea tena Ubunge Urambo ya Mashariki baada ya kuwa katika ulingo wa siasa kwa miaka 35 na badala yake ataangalia namna nyingine ya kuwatumikia wananchi huku akigusia mchakato wa kuwania urais ambao, alisema anamwachia Mungu.
 
“Kwa ubunge nimekwisha waeleza inatosha sitagombea tena kwani miaka 35 inatosha, … lakini hatima yangu ni nini siwezi kujua lakini nina afya nzuri na mmoja wa wanasiasa wakongwe, wenye afya nzuri, mnaona ninavyopendeza… kwa urais namwachia Mungu tutaona,” alisema Sitta.
 
Alisema yeye rafiki zake hao wana mawazo yanayolingana katika mustakabali wa nchi hii na kwamba wataendelea kutembea sehemu mbalimbali za nchi kuwajengea wananchi uelewa ili wajue kuwa uongozi ni lazima ukae katika mikono salama.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s