BIG BROTHER 2013: FEZA KESSY AONYWA KUHUSU NGONO

Feza Kessy.

Sifael Paul na Mitandao
LILE Shindano la Big Brother Africa 2013 ‘The Chase’ limeanza Jumapili iliyopita ambapo Tanzania inawakilishwa na mrembo ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Feza Kessy na modo wa kiume nchini, Ammy Nando ambapo watu wamemuonya mrembo huyo juu ya mambo ya ngono.
Mara baada ya kutajwa kwa jina la Feza ndipo watu wakaanza kudondosha maoni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya uwakilishi wake mjengoni humo.
Wadau hao walimuomba chondechonde asiwaaibishe kama akina Bhoke Egina ambao walihusishwa na mambo ya ngono huku wakirekodiwa na video zao kusambaa mitandaoni hadi leo.
“Chondechonde Feza usituchafulie sifa nzuri ya maadili yetu, wewe ndiye tafsiri halisi ya vijana wa Kitanzania,” aliandika Paul Kwere kwenye ukurasa wake wa Twitter.
“Usiwe kama wale wengine waliokwenda wakarudi na sifa mbaya, wakashindwa hata kutazama watu usoni kwa aibu,” aliandika Biashara Kwanza kwenye ukurasa wake wa Facebook.

WASIFU WA FEZA
Feza ni Mtanzania mwenyeji wa Arusha. Aliwahi kuwa Miss Dar City Center, Miss Ilala na Miss Tanzania namba 2 mwaka 2005, kabla ya hivi karibuni kujikita kwenye muziki na wimbo wake wa Amani ya Moyo akidaiwa kuwa kwenye ‘malavu’ na prodyuza wa Bongo Fleva aliyetajwa kwa jina moja la Lucci.

Ammy Nando.

WASIFU WA NANDO
Nando ni Mtanzania, mwenyeji wa Arusha ambaye ni modo wa kiume aliyeishi Marekani kwa muda mrefu kabla ya kurejea Bongo.
Katika shindano hilo, mwaka huu linajumuisha wawakilishi 28 kutoka katika nchi 14 ambapo kila nchi imepeleka wawili ambapo mshindi atachomoka na dola za Kimarekani 300,000 (zaidi ya Sh. milioni 480 za madafu).
Nchi hizo ni Kenya, Tanzania, Uganda, South Africa, Zambia, Zimbabwe, Nigeria, Angola, Ghana, Botswana, Malawi, Ethiopia na Sierra Leone.
Wafuatao ni baadhi ya washiriki wa mwaka huu na nchi zao kwenye mabano; Feza na Nando (Tanzania), Angelo (South Africa), Annabel na Huddah (Kenya), Betty na Bimp (Ethiopia), Basey na Bolt (Siera Leone), Beverly (Nigeria), Biguesas na Neyll (Angola), Cleo na Sulu (Zambia) na Fatima na Natasha (Malawi).
Wengine ni Hakeem na Pokello (Zimbabwe), Motamma na ONeal (Botswana), Selly na Elkem (Ghana), Dellish (Namibia) na Denzel (Uganda).

Advertisements

One Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s