ALIYEFUMANIWA NA DENTI… FAINI DOLA 400


Issa Mnally na Richard Bukos
YULE mfanyabiashara ‘alwatani’ wa jijini Dar ambaye hivi karibuni alifumaniwa gesti akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili, huenda akapandishwa kizimbani siku yoyote, Ijumaa Wikienda limeinyaka.
Kwa mujibu wa dada wa mwanafunzi huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, baada ya mfanyabiashara huyo kufumaniwa na binti huyo mwenye umri wa miaka 16, aliahidi kutoa fedha za Kimarekani dola 400 (zaidi ya Sh. 640,000) kama faini kwa kitendo hicho.
Hata hivyo, pamoja na kukubali kutoa kiasi hicho, mfanyabishara huyo hakutimiza ahadi yake na kuamua kuingia mitini.
Dada wa mwanafunzi huyo aliliambia Ijumaa Wikienda kwamba mfanyabiashara huyo anasakwa ili wamburuze mahakamani kutokana na mwisho wa mwezi uliopita kushindwa kutimiza ahadi yake.
“Aliandika kwa mkono wake kwamba atamlipa huyu mwanafunzi fedha hizo kama fidia ili akalipie ada ya kuendelea na masomo, lakini mpaka leo hii hajaonekana na wala simu yake ya mkononi haipatikani, tukimkamata tutamburuza mahakamani kwa sababu sheria hapa Bongo hazifuatwi kabisa kwani tulitarajia vyombo husika vingeingilia kati lakini hakuna lolote,” alisema dada huyo.
Aidha, dada huyo alisema kuwa wanatarajia kwenda kuchukua hati ya kumkamata mfanyabiashara huyo ‘RB’ katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ili waweze kumsaka.
“Ushahidi tunao tena wa uhakika kabisa, kaandika kwenye karatasi na katia saini yake, tena mwandishi naomba na zile picha alizopigwa akiwa chumbani na mdogo wangu ili zinisaidie katika ushahidi wa mahakamani,” alisema dada huyo huku akionesha karatasi ambayo waliingia makubaliano ya kulipwa dola hizo 400 na mfanyabiashara huyo.
Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu mfanyabiashara huyo alifumaniwa na denti huyo katika chumba namba 107 ndani ya gesti moja iliyopo Kinondoni, Dar na habari yake kuandikwa kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi la Aprili 27.Chanzo:www.globalpublishers.info

Advertisements

MATOKEO MABOVU YA KIDATO CHA NNE YATACHELEWESHA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA


 

 Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi  huu yatachelewa  ili kutoa nafasi kwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),  kurekebisha matokeo mabaya ya mitihani  kidato cha nne ya mwaka jana yaliyofutwa na serikali  mwezi huu.
 
Matokeo ya kidato cha sita ambayo huwa yanatangazwa mwanzoni  mwa mwezi Mei mpaka sasa hayajatolewa  na kwamba hayatatangazwa mpaka matokeo mapya ya kidato cha nne yatakaporekebishwa rasmi.

Alipoulizwa  juu ya suala hilo, Naibu Waziri   wa Elimu na  Mfunzo ya Ufundi  Philipo Mulugo alisema ingawa wakati huu ndio unaopaswa yatangazwe matokeo ya kidato cha sita haitafanyika hivyo hadi yatangazwe matokeo mapya ya kidato cha nne baada ya kufutwa.


Hata hivyo, akasema huenda yakatolewa  pamoja au yakafuata wakati mwingine lakini mara baada ya  kukamilisha kazi ya kurejea na kusahihisha matokeo ya kidato cha nne.


“Siyo kwamba yamechelewa kwani muda wa kujiunga na chuo ni Septemba hivyo haitawaathiri kwa hilo,” alisema Mulugo.


Kuhusu hatma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambao wapo mashuleni wanaendelea na masomo ya kidato cha sita, alisema  kama kutakuwa na wanafunzi ambao wapo madarasani  shule zilizowasajili  zitakuwa hazijafuata mfumo wa elimu unavyoelekeza.

Alifafanua kuwa mfumo wa elimu kwa kidato cha nne ulibadilishwa na kwamba endapo mwanafunzi akifaulu anatakiwa kujiunga rasmi kidato cha sita  Julai na si vinginevyo.

Alisema licha ya  ucheleweshaji  wa matokeo  hali hiyo haikuwaathiri wanafunzi hao kwa kuwa ratiba ya kwenda masomoni  haijaanza kwa mujibu wa kalenda  ya shule ya serikali.


Serikali ilifuta matokeo ya kidato cha nne ya 2012 na kuiagiza Necta kuyaandaa upya kwa kutumia utaratibu wa usahihishaji na upangaji madaraja uliotumiwa mwaka  2011

Taarifa ilisema mfumo uliotumika  mwaka jana na kusababisha wanafunzi kushindwa vibaya haukufanyiwa utafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika. 

Matokeo hayo  yaliyotangazwa  mwezi  Februari mwaka huu yalionyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi walishindwa mtihani.

9 Attributes Of The Best Entrepreneurial Leaders.


 

 

Creating and building a business is not a one-man show. It requires a team effort, or at least the ability to build trust and confidence among key players, and effectively communicate with partners, team members, investors, vendors, and customers. These actions are the hallmark of an effective leader.

 

Behind the actions are a set of principles and characteristics that entrepreneurial leaders, like Bill Gates and Steve Jobs, seem to have in common. Look for these and nurture them in your own context to improve the odds of success for your own start up:

 

1. Clarity of vision and expectations. You must be able and willing to communicate to everyone your vision, goals, and objectives. Just as importantly, you have to be absolutely clear about who you are, what you stand for, and what you expect from everyone around you. People won’t follow you if they are in the dark or confused.

 

2. Willingness to make decisions. It is often said that making any decision is better than making no decision. Even better than “any decision” is a good decision made quickly. Business decisions always involve risk, at times a great deal of it. Smart entrepreneurs always balance the risk with facts, when they have them, rather than their gut.

 

3. Experience and knowledge in your business area. Effective leaders set a personal standard of competence for every person and function in the start up. It must be clear that you have the knowledge, insight, and skill to make your new company better than your very best competitor.

 

4. Commitment and conviction for the venture. This commitment must be passionate enough to motivate and inspire people to do their best work, and put their heart into the effort. Behind the passion must be a business model that makes sense in today’s world, and a determination to keep going despite setbacks.

 

5. Open to new ideas and creativity. In business, this means spending time and resources on new ideas, as well as encouraging people to find faster, better, cheaper, and easier ways to produce results, beat competition, and improve customer service. Be a role model and guide others to excel.

 

6. Courage to acknowledge and attack constraints. An effective leader is willing and able to allocate resources to remove obstacles to the success of the start up, as well as removing constraints on individuals on the team. It is believing that where there is the will, there will be a way.

 

7. Reward continuous learning. You have to encourage everyone to learn and grow as a normal and natural part of business. That means no punishment for failures, and positive opportunities for training and advancement. Personally, it means upgrading your own skills, listening, and reading about new developments and approaches.

 

8. Self-discipline for consistency and reliability. An effective leader is totally predictable, calm, positive, and confident, even under pressure. People like to follow someone when they don’t have to “walk on eggshells” to avoid angry outbursts, or assume daily changes in direction.

 

9. Accept responsibility for all actions. Everyone and every company makes mistakes. Good entrepreneurs don’t want to be seen as perfect, and they have to be seen as willing to accept the fact that “the buck stops here.” No excuses, or putting the blame on the economy, competitors, or team members.

 

The good news is that all of these principles of leadership are learnable. The bad news is that it’s not easy. Don’t assume that success as an entrepreneur is only about great presentations, killing competitors, or having insanely great ideas. It’s really more about leadership, understanding the needs of your prospective clients, and communicating your solutions with clarity.Source:moeblog

Lady Jay Dee kuripoti Mahakama ya Kinondoni kesho


 

 

 

jd 36b09

Na Andrew Chale
MWANAMUZIKI nguli wa bongo na kiongozi wa yenye mvuto nchini bendi ya ‘Machozi’, Judith Wambura ( Lady JayDee) au Jide ama #Teamaanaconda#, anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni siku ya Jumatatu Mei 13, kufuatia kufikishiwa kwa taarifa hizo Gadna G Habash ‘Captain’ ambaye ni Meneja na mume wa Lady Jay Dee. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mchana wa leo, Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa kwa Lady Jay Dee kufika Mahakama ya Kinondoni, siku ya Jumatatu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni, Hii ni kufuatia kwa jana kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo na walikuja na barua ya kumkabidhi Lady Jay Dee mwenyewe hata hivyo hawakumkuta” alisema Gadna.
Aliendelea kueleza kuwa, hata alipowaeleza watu hao wamkabidhi yeye hiyo barua watu hao walisema ilikuwa si lahisi zaidi alitakiwa akabidhiwe mlengwa, hivyo kumueleza kuwa wito wa kufika mahakamani siku ya Jumatatu, na aliwakubalia kwa hilo.
Hata hivyo, Gadna alisema hajajua Lady Jay Dee anaitiwa nini na kwa sababu ya nani zaidi amemwelezea na amesema watatekeleza wito huo wa kufika Jumatatu Mahakamani hapo.
Aidha, kupitia kwenye ukurasa wake wa Kijamii wa facebook, Lady Jay Dee aliandika: “Ratiba ya Usiku wa leo, ni Machozi Band, kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea…” aliandika Jide kwenye ukurasa huo ambao mpaka hatua ya mwindishi anatembelea ‘post’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ambayo watu mbalimbali walipata kuchangia.
Maoni hayo yanayokaribia zaidi ya 558 na, ‘Like’ zaidi ya 756 na ‘Share’ zaidi ya 20, ambapo wengi wao wameweza kumuhusisha moja kwa moja na Mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba kuwa ndie aliyefanya hivyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali na moja ya gazeti hivi karibuni ilimnukuu Ruge kuwa amejiandaa kuchukua hatua ikiwemo ya kisheria dhidi ya Lady Jay Dee baada ya kumsema kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

KAMANDA KOVA AKANUSHA TAARIFA ZA KULIPULIWA KWA KANISA LA KKKT KUNDUCHI


 

 

KAMANDAKOVAJeshi la polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam  limekanusha taarifa zilizozagaa kuwa kanisa la KKKT Usharika wa  Kunduchi  limelipuliwa na bomu leo hii.Kamanda Suleiman Kova ameiambia radio Uhuru Fm kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na ni za uzushi kwani jeshi la Polisi lilirusha bomu la machozi wakati likitafuta waharifu waliokuwa jirani na kanisa hilo.

TASWIRA KUTOKA IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA KIKAO CHA SADC CAPE TOWN


 

  Rais Dk. Jakaya Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Misaada la Marekani USAID, Dk. Rajiv Shah muda mfupi baada ya kufanya naye mazungumzo katika Ukumbi wa Cape Town Convention Center jana
 Rais Kikwete na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika Kusini wakitoka katika ukumbi wa hoteli ya Westin jijini Cape Town Afrika ya Kusini mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalma ya SADC kilichofanyika leo. Rais Kikwete alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC Rais Kikwete, akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Dk..Tomaz Salomao jijini Cape Town, Afrika ya Kusini leo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
  Rais Kikwete (wa tatu kushoto) akiongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC kilichofanyika jijini Cape Town Afrika Kusini leo.Wengine katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo akiwemo mwenyeji Rais Jackob Zuma wa Afrika Kusini (kulia), Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Namibia Bibi Netumbo Nandi-Ndaitwa (kushoto), na wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dk. Tomaz Salomao.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji na Mratibu wa Asasi ya Bill and Melinda Gates Foundation, Mark Suzman jijini Cape Town, Afrika ya Kusini. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Adam Malima.Picha na Freddy Maro-IKULU

Multichoice Tanzania yajikita katika kusambaza Digitali katika shule za msingi Tanzania.


 

 

 

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akiwakaribisha wageni wanahabari katika hafla mchapalo ya kusheherekea Africa Day na Dstv ambapo amesema DStv inatoa nafasi kwa wateja wake kuwa na fursa ya kuchagua vifurushi mbalimbali kulingana na uwezo wa mteja ambacho cha uwezo wa chini kabisa ni Access chenye zaidi ya channeli 40 gharama yake ni nafuu sana ambapo mteja atalipia shilingi 16,500 kwa mwezi. (Picha na Zainul Mzige wa dewjiblog).

 

 

 

 

Meneja wa Fedha wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Bw. Francis Senguji akizungumzia malengo ya DStv Tanzania ambapo amesema wao kama waendeshaji wa biashara nyingine barani Afrika wanaojali na kuthamini maendeleo ya jamii wameona ni wajibu kusaidia jamii ili kuweza kuendeleza maendeleo ya kijamii nchini Tanzania.

 

 

 

Kwa kuendeleza hilo Multichoice ina mfumo wa kutoa elimu mashuleni ( Multichoice Resource Centre) hivyo watamumia jukwaa la Teknolojia kama darasa kwa njia mbalimbali kuwapa jamii nafasi ya kuendeleza vipaji na ujuzi.

 

 

 

Mfumo huo kutoa rasilimali kwenye shule kama vile ving’amuzi vya Satellite, VCRs/DVD na kifurushi cha elimu cha Dstv. Mpaka sasa Multichoice imeanzisha vituo vya rasilimali jamii katika shule 82 nchi nzima kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Mbeya, Pwani na Tanga.

 

 

 

 

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) akifafanua jambo wakati wa hafla mchapalo katika kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Barbara Kambogi.

 

 

 

 

Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Blogger John Bukuku wa Fullshangwe Blog, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo Ronald Shelukindo, Mdau wa DStv na Meneja wa Fedha katika kampuni hiyo Bw. Francis Senguji wakipozi kwa picha.

 

 

 

Kwa taswira zaidi tembelea Mo.blog