Kocha Mkuu wa Uingereza Hodgson afurahishwa kutoka sare ya magoli 2-2 dhidi ya Brazil

Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amewasifu wachezaji wajke kwa namna ambavyo wamecheza katika kipindi cha pili cha mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Brazil uliopigwa katika Dimba la Maracana.
 
Nice hit: Rooney also played a part in Alex Oxlade-Chamberlain's stunning strike - could they now be team-mates at Arsenal?
Wachezaji wa Uingereza Wayne Rooney na Frank wakishangilia goli lililofungwa na Alex Oxlade-Chamberlain katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil
 
Hodgson amekiri licha ya kucheza vibaya katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo lakini walifanikiwa kuonesha kiwango na uwezo wao katika kipindi cha pili cha mchezo huo na kufanikiwa kupata matokeo ya sare ya magoli 2-2.
 
Kocha huyo amesifu sana namna ambavyo safu ya ulinzi ya Uingereza ilivyoweza kuwabana wachezaji wa Brazil ambao walikuwa mwiba katika muda mwingi wa mchezo huo hasa kipindi cha kwanza.
 
Hodgson hakuwa mchoyo wa fadhila pale ambapo alikiri kuingia kwa Alex Oxlade-Chamberlain kulisaidia pakubwa kubadili mwelekeo wa mchezo huo ambapo alifanikiwa kufunga goli la kusawazisha.
 
Brazil ilikuwa ya kwanza kupata goli katika mchezo huo uliopigwa kwenye Dimba la Maracana kupitia Mshambuliaji wake Fred goli ambalo lilisawazishwa na Oxlade-Chamberlain aliyefunga goli kwa ufundi mkubwa.
 
Wonder goal: Rooney smashed home England's second goal of the night against Brazil at the Maracana
Uingereza ilipata goli la pili kupitia Wayne Rooney ambalo walidhani lingetosha kuwapa ushindi kwenye mchezo huo huko Maracana lakini ndoto zao zilizimwa kwa goli la Paulinho na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare.
 
Kocha Mkuu wa Brazil maarufu kama Samba Boys Luiz Felipe Scolari amesifu wachezaji wake kwa namna walivyocheza na kusema walicheza na watu wenye uzoefu mkubwa waliotumika timu ya Uingereza Three Lions kwa muda mrefu.
 
Scolari amesema ni matokeo mazuri kwa vijana wake ambao wanajiandaa kwa mashindano ya Kombe la Mabara yatakayofanyika nchini Brazil baadaye mwezi wa sita na anaamini mchezo huo utakuwa umewasaidia kuona mapungufu yao.
 
Huu ulikuwa mchezo wa pili baina ya Samba Boys na Three Lions kwani katika mchezo wa kwanza uliopigwa mwezi Februari katika Dimba la Wembley ulishuhudia Uingereza wakiwachakaza Brazil kwa magoli 2-1. Via kiswahili.rfi.fr
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s