Maalim Seif awakumbusha wakaazi wa Arusha kuitunza amani iliyopo

 

 

 

Na Hassan Hamad OMKR
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amewatahadharisha wakaazi wa Arusha kuilinda na kuitunza amani iliyopo ili kuuendeleza mji huo kiuchumi.
 
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimtambulisha mgombea udiwani kata ya Themi mkoani Arusha, Lobora Petro Ndarpoi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya relini kata ya Themi.
 
Amesema mji wa Arusha ni miongoni mwa miji muhimu katika maendeleo ya Tanzania kutokana na umaarufu wake na kuwa mji wa kitalii na biashara.
 
Maalim Seif ametoa tahadhari hiyo katika kata za Themi na Kaloleni mjini Arusha, wakati akiwahutubia wakaazi wa maeneo hayo kwenye mikutano ya kampeni za udiwani katika kata hizo.
 
Amefahamisha kuwa mji huo umeiletea sifa kubwa Tanzania na kupelekea kuwa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kituo muhimu cha mikutano ya kimataifa.
 
Ameongeza kuwa iwapo amani itatoweka katika eneo hilo, itaupotezea sifa mji huo na kushuka kwa mvuto wake wa kitalii, kibiashara na shughuli za kimataifa.
 
Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema wakaazi wa Arusha wana kila sababu ya kujivunia maendeleo na rasilimali zilizopo, yakiwemo madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Arusha pekee duniani kote.
 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s