MAMA MZAZI WA PROFESA J AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI DAR

Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake.  Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya ‘Aluta Continua’.

Habari zilizotufikia ni kwamba Mama Mzazi wa Msanii mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya, Joseph Haule ‘Profesa J’ amefariki dunia jana usiku kwa kugongwa na gari. Marehemu Bi. Rosemary Majanjara Haule aligongwa na gari wakati anavuka barabara kuelekea dukani majira ya saa mbili usiku na baada ya kugongwa wasamaria wema walimkimbiza hospitali ya Tumbi ambapo alipoteza maisha.

Profesa J amethibitisha habari hizi kwa kusema kuwa, inamuwia vigumu kuamini kilichotokea kwani mnamo majira ya saa mbili usiku marehemu alimpigia simu na kumweleza kuwa amepata ajali na kwamba wakati huo alikuwa kituo cha polisi  bila shaka kupata PF3 kwa ajili ya matibabu.
“Mama aliniambia, mwanangu nimegongwa na gari…. njoo niko polisi naandikisha….mwanangu nakufa…. Aliniambia mama na mara simu ikakatika. Kila nilipojaribu kupiga simu ikawa haipatikani…” Alisema Profesa J kwa uchungu.

Global Publishers Ltd inatoa pole kwa msanii Profesa J pamoja na wanafamilia wote. Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN!
Chanzo: Michuzi Blog

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s