KIPANYA LEO


 

kp022014_53f37.png

 Pia unaweza kuzama…www.kingkif.blogspot.com
 
Advertisements

DRC YAPUUZA OMBI LA ICC LA KUMKAMATA AL-BASHIR


 

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepuuzilia mbali ombi la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC la kuitaka imtie mbaroni Rais Omar al-Bashir wa Sudan. 
 
Rais Omar al-Bashir wa Sudan. 
 
Jana Mahakama hiyo ya Jinai ya ICC sambamba na kutoa waranti wa kutaka kutiwa mbaroni al-Bashir, iliitaka serikali ya Kongo, kuharakisha kumkamata rais huyo wa Sudan aliyewasili katika mji mkuu wa Kongo Kinshasa kwa lengo la kushiriki kikao cha wakuu wa nchi za Kiafrika, na kumkabidhi kwa mahakama hiyo ya jinai. 
 
Hata hivyo serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ilipuuzilia mbali ombi hilo. Katika mwaka 2009 na 2010, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa waranti wa kutiwa mbaroni Rais Omar al-Bashir wa Sudan kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binaadamu na mauaji ya umati katika mapigano yaliyowahi kutokea Darfur, Sudan. 
 
Hata hivyo licha ya kutolewa waranti huo dhidi yake, al-Bashir, amekuwa akifanya safari nje ya nchi bila khofu yoyote. 
 
Hii ni kwa sababu viongozi wengi wa nchi za Afrika wamekuwa wakikosoa mwenendo mzima wa mahakama hiyo ya ICC na kusema kuwa, mahakama hiyo inaendeshwa kisiasa kwa kuwasakama viongozi pekee wa bara la Afrika.
 

WABUNGE CCM WAJILIPUA


 

Dodoma/Dar. Wajumbe watatu wa Bunge la Katiba ambao ni wabunge wa CCM wametofautiana na msimamo wa chama chao kwa kuunga mkono kura ya siri itumike kuamua ibara za Rasimu ya Katiba.
 

Mjumbe wa Bunge la Katuba,Profesa Juma Kapuya.PICHA|MAKTABA

Hilo lilitokea jana katika mjadala mkali baina ya wajumbe kuhusu ama matumizi ya kura za siri yatumike au kura za wazi.
 
Katika mjadala huo ulioonyesha mgawanyiko wa wazi, wajumbe wengi wanaotokana CCM na ambao wamekuwa wakipigania kura za wazi, walionekana kuwazidi kwa wingi wale wanaotaka kura za siri.
 
Wajumbe wa CCM ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muunganom– Esther Bulaya na Profesa Juma Kapuya walijitoa mhanga na kueleza bayana kuwa hawako tayari kuona demokrasia ikikandamizwa kwa kulazimishwa kupiga kura za wazi. Akishangiliwa kwa nguvu, Bulaya alisisitiza kuwa hayuko tayari kulazimishwa kupiga kura ya wazi huku akijua kuwa utaratibu huo unamnyima uhuru wake.
 
“Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. Ni lini na wapi maamuzi magumu kama haya yalifanyika?” Alihoji mbunge huyo wa Viti Maalumu.
 
Bulaya alisema hakuna sheria inayomtaka mtu kushurutishwa kufanya uamuzi na kwamba kumtaka atoe sauti ya juu katika kura za wazi, ni kumlazimisha kufanya kinyume na matakwa yake.
 
 

JOKATE ULOKOLE BASI!


 

Stori: Hamida Hassan
Picha za nusu utupu ambazo amezipiga mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo zinaonekana kumtesa kufuatia baadhi ya waumini wa kanisa analosali kumsema kuwa anakwenda kinyume na maadili.
Picha hizo anazoonekana amevaa gauni refu jekundu huku likiwa na mpasuo ‘wa haja’ uliyolifanya sehemu kubwa ya paja lake kuwa wazi, zimesambaa kiasi cha kuwafanya baadhi ya mashabiki wake kumtaka ajiangalie upya.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wamesema kutokana na jinsi alivyokuwa ametulia kiimani, mrembo huyo alikuwa anaelekea kwenye ulokole lakini kwa hili anapotea.
“Unajua yule ni modo mwenye jina kubwa sana lakini alikuwa ametulia sana, hata nilipomuona amejiunga na kwaya ya pale kanisani kwetu St. Peter, niliona ameamua kumfuata Yesu kikwelikweli lakini kwa picha hizi, mh!” alisema Juster John anayesali kanisani hapo.
Naye rafiki wa Jokate aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema: “Ninachokumbuka Jokate aliwahi kuniambia anataka kuokoka ili amtumikie Yesu kisawasawa lakini kwa mavazi haya nadhani mawazo ya ulokole itakuwa basi tena.”
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Jokate na kumuuliza juu ya picha hizo, alipopatikana alisema: “Nilizipiga kwa ajili ya kuitangaza kampuni yangu ya mitindo ya Kidoti.
Ijumaa: Sasa mbona umeacha mapaja wazi sana?
Jokate: Huh!
Ijumaa: Huh nini?
Jokate: Nishasema ni za Kidoti, ilikuwa ni kwa ajili ya kutangaza nguo na nywele zangu.
Ijumaa: Kuokoka ndiyo basi tena?
Jokate: Kimyaaa.
Hata hivyo gazeti hili linamshauri mrembo huyu kwamba, kwa kuwa ameshajijengea heshima kubwa kwenye jamii, ni vyema akawa makini na mavazi kama haya ambayo yanaweza kumfanya akatafsiriwa tofauti.Chanzo:www.globalpublishers.info