DRC YAPUUZA OMBI LA ICC LA KUMKAMATA AL-BASHIR

 

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepuuzilia mbali ombi la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC la kuitaka imtie mbaroni Rais Omar al-Bashir wa Sudan. 
 
Rais Omar al-Bashir wa Sudan. 
 
Jana Mahakama hiyo ya Jinai ya ICC sambamba na kutoa waranti wa kutaka kutiwa mbaroni al-Bashir, iliitaka serikali ya Kongo, kuharakisha kumkamata rais huyo wa Sudan aliyewasili katika mji mkuu wa Kongo Kinshasa kwa lengo la kushiriki kikao cha wakuu wa nchi za Kiafrika, na kumkabidhi kwa mahakama hiyo ya jinai. 
 
Hata hivyo serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ilipuuzilia mbali ombi hilo. Katika mwaka 2009 na 2010, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa waranti wa kutiwa mbaroni Rais Omar al-Bashir wa Sudan kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binaadamu na mauaji ya umati katika mapigano yaliyowahi kutokea Darfur, Sudan. 
 
Hata hivyo licha ya kutolewa waranti huo dhidi yake, al-Bashir, amekuwa akifanya safari nje ya nchi bila khofu yoyote. 
 
Hii ni kwa sababu viongozi wengi wa nchi za Afrika wamekuwa wakikosoa mwenendo mzima wa mahakama hiyo ya ICC na kusema kuwa, mahakama hiyo inaendeshwa kisiasa kwa kuwasakama viongozi pekee wa bara la Afrika.
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s