Become a website & graphics designer in just 4 Saturdays in April


 

 

In today’s digital era, the way organizations do business is rapidly changing. Today, professionals help organizations to create their internet web presence, reaping huge profits for organizations by reaching out to more customers and spreading awareness of their products.

The training for ‘Website Design’ will enable you to maximize internet opportunities to help organizations become even more successful. It’s your chance to embark on this profitable and ever involving world of unlimited opportunities without prior web knowledge or coding or programming. Continue…

Advertisements

RED CROSS YAPIGWA JEKI KUWASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO KILOSA


 

Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale,  akifurahia jambo wakati akipokea mfano wa hundi ya Shilingi Milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii” Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule. Fedha hizo zimetolewa kwa chama hicho kwa ajili ya kuimarisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro na kuacha mamia ya kaya bila makazi. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Julius Kejo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalimu.
Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale,  akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) punde baada ya kupokea msaada wa fedha, kiasi cha Shilingi milioni kumi kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii”Vodacom Foundation” kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Pamoja nae katika picha kutoka Kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.
Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale na Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzanaia”Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule, wakimsikiliza mmoja wa Maafisa wa Tanzania Red Cross punde baada ya kupokea msaada wa fedha kiasi cha Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo hicho  kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro
Mkuu wa Kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania” Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule akizungumza na  waandishi wa Habari (Hawapo pichani) punde baada ya kutoa msaada wa fedha kiasi cha Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na kitengo hicho”Vodacom Foundation”kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Pamoja nao katika picha ni Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale (katikati)Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.

Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania”Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule akizungumza na baadhi ya maafisa wa Tanzania Red Cross, punde baada ya kufanya makabidhiano ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni 10 ambazo zitasaidia kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Red Cross yapigwa jeki kuwasaidia wahanga wa mafuriko Kilosa

Dar es Salaam, Tanzania Red Cross  leo imepokea msaada wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kuiwezesha kuimalisha huduma na kusaidia waaliokumbwa na maafa ya mafuriko wilayani kilosa Mkoani Morogoro.

 Itakumbukwa kwamba mnamo tar. 22-23,Januari 2014, mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kutokea ndani ya kipindi cha miaka 15, yalikumba wakazi wa eneo la Dumila, kuwaacha mamia ya wakazi wakiwa hawana sehemu za kuishi, chakula cha uhakika huku miundombinu mbali mbali ya kiuchumi na kijamii ikiwa imeharibiwa vibaya.

Tathmini iliyofanywa na Serikali ya Mkoa wa Morogoro inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 9,000 waliathirika kwa namna na viwango mbalimbali. Mafuriko haya ya ghafla (Flash Flood) yalisababishwa na mvua zilizonyesha katika nyanda za juu za mikoa ya jirani ikiwemo Dodoma, Tanga na Manyara.   Wilaya ya Kilosa ndiyo iliyopata madhara makubwa zaidi kutokana na janga hili ambapo takribani watu 7,600 waliathirika na nyumba zaidi ya 500 kubomoka kabisa na hivyo  familia husika kukosa nyumba za kuishi.  Wilaya nyingine  zilizoathirika ni pamoja na Gairo (waathirika 958), Mvomero (690) .

 Akizungumza wakati wa makabidhiano wa msaada huo Mkuu wa Kitengo cha mfuko wa kusaidia jamii “Vodacom Foundation” Bw. Yessaya Mwakifulefule alisema kuwa matumaini ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dumila yapo kwetu sisi watanzania kujitoa kwa hali na mali kuwarejeshea maisha yao ya awali.

“Kwa kuitambua Tanzania Red Cross kwa majukumu yake katika kuisaidia jamii kwa kukabiliana na maafa, leo tunakabidhi kiasi hiki cha fedha kwa chama cha msakaba mwekundu nchini kuhakikisha dhamira yake ya kusaidia umma wa watanzania katika wakati mgumu kama huu.” Alisema Mwakifulefule

 Rais wa Tanzania Red Cross, Dr.George Nangale, amesema baada ya maafa hayo, chama kilichukua hatua za haraka kwa kutoa msaada wa mahitaji ya dharura kama vile, vyandarua (300), mablanketi (300) na ndoo za maji (300) na madumu ya maji (160) Msaada huu wa awali uliwafikia walengwa katika kipindi cha saa 24 baada ya maafa kutokea.

“Bada ya maafa hayo, chama kilichukua hatua za haraka kwa kutoa msaada wa mahitaji ya dharura kama ilitolewa katika kipindi cha saa 24 baada ya maafa kutokea. Kilichofuata ni tathimini ya awali iliyoonyesha kwamba mbali na mahitaji mengine, makazi ya dharura yalikuwa hitaji muhimu na haraka kutokana na ukweli kwamba familia nyingi zilipoteza nyumba zao” amesema Nangale.

Aliendelea kusema kwamba kwa ufadhili wa shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu Duniani(IFRC), Tanzania Red Cross imeweza kujenga nyumba za dharura kwa ajili ya familia 400 zilizokuwa na uhitaji mkubwa .

Nangale aliendelea kusema kwamba makazi haya ya muda yamegharimu kiasi cha jumla ya shilingi 80,000,000/=(Milioni Themanini).  Mahitaji mengine yanayoendelea kutolewa ni pamoja na magodoro (800), vyombo vya jikoni (seti 400), madumu ya maji (500) sabuni za kufulia, vyandarua, mablanketi, huduma za ushauri/ nasaha(pysco social support), na elimu ya afya na mazingira, vyote hivi vikiwa na thamani ya  takribani shilingi 96,600,000/=. Ufadhili huu umetolewa na IFRC,Shirika la Umoja wa Maitaifa la UNICEF na kampuni Vodacom.

 “Tunawashukuru sana Vodacom na wengine wote waliotuwezesha katika harakati za kutimiza wajibu wetu kwa jamii hasa katika wakati huu wa maafa yaliyotokea huko Morogoro.  Tunatoa wito kwa Taasisi mbalimbali pamoja na watanzania wote kwa ujumla kujenga na kuendelea na moyo wa kupenda kusaidia pale yanapotokea maafa kama haya na mengineyo”, amesema Rais wa Tanzania Red Cross.

 

aarifa Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu:Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Maji itafute njia mbadala zitazosaidia kupunguza gharama za kuchimba visima ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.


 

 

 

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa maji wa Mkonze katika Maanispaa  ya Dodoma katika kilele cha wiki ya maji Machi 22, 2014. Kushoto kwake ni Waziri wa Maji, Profesa  Jumanne Maghembe

 

 

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa maji wa Mkonze katika Maanispaa  ya Dodoma katika kilele cha wiki ya maji Machi 22, 2014. Kulia ni Waziri wa Maji, Profesa  Jumanne Maghembe.

 

 

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimtwika maji, Bibi Edna petro baada ya kuzindua mradiwa maji wa Mkonze katika Manispaa ya Dodoma ikiwa ni moa ya shughuli za kilele cha wiki ya maji  Machi 22, 2014

 

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya kuweka jiwe la msingi la  mradi wa tangi la maji  ikiwa ni moja ya Shughuli za kilele cha wiki  ya maji  Machi 22, 2014.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MWANDISHI UINGEREZA AIBUA MAPYA MENO YA TEMBO


 

Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ahadi ya kuteketeza maelfu ya meno ya tembo yaliyo kwenye ghala la Serikali, imeelezwa kuwa uwezekano huo ni mdogo.

Mwandishi wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Martin Fletcher ameeleza kushtushwa na hali ya ulinzi kwenye ghala hilo lililosheheni meno 34,000 ya tembo ambayo kwa biashara ya magendo nchini China yanagharimu Pauni 150 milioni za Kiingereza (Sh403.5 bilioni)

Fletcher, ambaye aliandika habari ya kuhusika kwa wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wa Tanzania katika biashara haramu ya meno hayo kiasi cha kuifanya nchi kuwa muuzaji mkuu wa nyara hizo, aliandika hayo kwenye taarifa kuhusu ziara yake nchini iliyochapishwa na gazeti hilo jana.

Habari ya awali ilitikisa ulimwengu ambao unapambana kulinda viumbe walio hatarini kutoweka ikiwatuhumu wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa nchini kuhusika, huku Serikali ikishindwa kuwadhibiti.(P.T)

Read more…

 

 

 

KATIBU WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AWATAKA WAJUMBE KUWEPO KWENYE VIWANJA VYA BUNGE LEO MCHANA


 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

ngaoBUNGE MAALUM 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu wa Bunge Maalum Bwana Yahaya Khamis Hamad anawatangazia Wajumbe wote wa Bunge Maalum kuwa wafike kwenye viwanja vya Bunge leo saa 8:45 mchana ili kushiriki kikao cha Bunge Maalum kitakachoanza saa 9:00 mchana na kufuatiwa na hutuba ya ufunguzi wa Bunge Maalum itakayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete saa 10 jioni. Kwa maelezo zaidi piga 0713 123 254.

Imetolewa na Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum

DODOMA

21/03/2014

RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014


 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dodoma leo kwa ratiba ifuatayo:

Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa.

Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum leo saa 2:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.

Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.

Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.

Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania.

Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge Maalum na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum Atakaye ipata taarifa hii amjulishe mwenzake.

Imetolewa na Ofisi ya KATIBU WA BUNGE

 

 

 

Kutoka Wizara ya Waziri Mkuu:Waziri Mkuu Mizengo Pinda Azindua Rasmi Tovuti ya Taasisi ya Figo nchini baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya Afya ya figo kwenye viwanja wa Nyerere mjini Dodoma


 

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Tovuti ya Taasisi ya Figo nchini baada ya kuhutubia katika  maadhimisho ya kilele cha wiki ya Afya ya figo kwenye viwanja wa Nyerere mjini Dodoma  Machi 13, 2014.
 Waziri Mkuu, MIzengo Pinda akizungumza  na watalaamu wa magonjwa ya figo katika maadhimisho  ya kilele cha wiki ya Afya  ya Figo, kwenye viwanja vya Nyerere mjini Dodoma Machi 13, 2014.Kutoka kushoto ni  Dr. Tulizo Sanga wa Muhimbili, Kulindwa Kasubi wa Muhimbili na Regina Ringo  wa Hospitali ya Mirembe ya Dodoma. Katikati ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa  wa Taasisi ya Taifa ya Figo Tanzania Jaji Frederick Werema na kushoto kwake ni Dr. Linda Ezekiel kutoka Wizara ya Afya.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na baadhi ya viongozi baada ya kuhutubia  katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya Afya ya  Figo kwneye  viwanja vya Nyerere mjini Dodoma Machi 13, 2014. Kushoto ni Naibu Waziri  wa Afya, Dr. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa serikali na  Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Figo, Jaji Frederick Werema.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu