WAWAKILISHI WA ZANZIBAR WAHOJI BARAZA LAO..

 

Wajumbe wa Bunge la Katiba.

Wakati Bunge Maalumu la Katiba, likitarajiwa kukutana leo kuamua kura gani itumike katika uamuzi wa mwisho wa kupitisha Katiba itakayopendekezwa kwa wananchi, wawakilishi wanachama wa CCM, wameibuka na kuhoji maoni ya Baraza la Wawakilishi kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 
Maoni hayo yalichapishwa jana katika magazeti, yakionesha kuwa Baraza la Wawakilishi limetoa msimamo wa pamoja, kuashiria kutaka muundo wa Muungano wa serikali tatu.
 
Mbali na muundo huo, pia inadaiwa maoni ya baraza hilo yalipendekeza Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ya nchi na Tanganyika iwe na mamlaka kamili.
 
Jana Katibu wa Kamati ya Wawakilishi wa CCM, Salmin Awadh Salmin, aliitisha mkutano na waandishi wa habari mkoani hapa na kukanusha kuhusika kwao katika maoni ya Baraza yaliyowasilishwa katika Tume.
 
Katika mkutano huo wa dharura, Salmin alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliomba taasisi mbalimbali, ikiwemo Baraza la Wawakilishi, kupeleka maoni yake kuhusu Katiba mpya.
 
Hata hivyo, Salmin alisema walijua kuwepo kwa mwaliko huo, lakini baada ya hapo kilichoendelea kilikuwa siri ambapo baadhi wa wawakilishi wakiwemo viongozi wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wawakilishi, hawakushirikishwa.
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s