‘PANDU KIFICHO AMETUSALITI’

Zanzibar. Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho amekiri kuwasilisha waraka kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba na kupendekeza Zanzibar na Tanganyika kuwa na mamlaka huru, hatua ambayo imezua malalamiko miongoni mwa makada wa chama hicho ambao wamesema huo ni usaliti.

 
Mnadhimu Mkuu wa CCM kwenye Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin akizungumza jana mjini Dodoma kuhusu kutotambua maoni ya Baraza la Wawakilishi yaliyopelekwa na kwenyeTume ya Mabadiliko ya Katiba. Kushoto ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, Shamsi Vuai Nahodha. Picha na Emmanuel Herman 

Akizungumza kwa simu kutoka Dodoma, Kificho ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), alisema kimsingi waraka huo ulilenga kuipa nguvu Zanzibar kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano ili kujiimarisha kiuchumi.

 
Kauli ya Kificho inakuja wakati baadhi ya wajumbe wa CCM kutoka Zanzibar wakiitisha mkutano na kutoa tamko la kumshutumu kwa kutoa mapendekezo hayo, wakisema ni kinyume na msimamo wa chama hicho.
 
Kificho alionyesha kushangazwa na madai kuwa mapendekezo hayo yaliyoandaliwa na watu wanne ambayo ameyasaini si msimamo wa BLW.
 
“Tatizo lililopo ni tafsiri ya kila mmoja anapousoma waraka huo, hakuna sehemu tuliyoandika tunataka Serikali tatu, mamlaka huru maana yake kila upande uwe na uwezo wa kushughulikia mambo yake yasiyo ya Muungano na kujijenga kiuchumi, ikiwa ni pamoja Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa (OIC) na siyo kuunda dola,” alifafanua Spika Kificho.
 
Alisisitiza kuwa angependa mambo ambayo hayamo katika orodha ya Muungano yaendeshwe na Zanzibar bila ya kuwekewa vikwazo mahali popote.
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s