HATI YA MUUNGANO KUTUMIKA KATIKA BUNGE MAALUM

 

mnyika-john_89cc9.jpg

John Mnyika

HATI ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni miongoni mwa nyaraka ambazo Bunge Maalum la Katiba, limekubali kuwa kiwe ni moja ya vielelezo, ambavyo Wajumbe watavitumia watakapokuwa wanachangia hoja zinazohusu jambo hilo.

Makubaliano hayo yalikuja baada ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema) kuwasilisha marekebisho katika kipengele kinachohusu haki na kinga ya Bunge Maalum ambako aliongezea kipengele cha kutaka wabunge wapewe haki ya kupewa nyaraka watakazohitaji ambazo zilitumiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Katika mchango wake, Mnyika alisema kwamba katika orodha ya nyaraka ambazo zimeorodheshwa kutumiwa na wabunge hao kwa ajili ya kuboresha michango yao, hati ya Muungano haipo na akasema kuwa kwa vile nyaraka hizo zilitumiwa na Tume ya Warioba ni vyema wabunge nao wapewe kinga ya kuitumia ili kuboresha michango yao watakayowasilisha bungeni.

Hoja hiyo ilikubaliwa na Kamati ya Kanuni baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othuman Masoud kusimama na kusema anakubaliana na marekebisho hayo ya Mnyika.

Lakini, Mbunge wa Simanjiro Christopher ole Sendeka alisimama na kupinga suala hilo kwa maelezo kuwa Hati ya Muungano ni hati ambayo ina kinga haiwezi kutumiwa na wabunge hao na akaeleza hatari ya kutumia hati hiyo.

Sendeka alisema kuna nyaraka ambazo ni lazima ziletwe kwenye Bunge la Katiba ambazo ni kama muhtasari wa maoni ya wananchi, mapendekezo ya wataalamu elekezi, Rasimu ya Katiba na taarifa nyingine muhimu na sio Hati ya Muungano.

CHANZO:HABARILEO

(MM)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s