URUSI YAIONYA MAREKANI DHIDI YA VITISHO VYA KUIWEKEA VIKWAZO VYA KIUCHUMI NA KWAMBA INAUWEZO WA KUJIKUMU PEKEAKE

Na Ali Bilali

 
Nchi ya Urusi imeionya serikali ya Marekani dhidi ya hatua yoyote iliyopanga kuchukua ikiwa ni pamoja na kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuongeza kuwa atakaeumia kwenye mzozo huo atakuwa ni Marekani mwenyewe. 
 
Vladimir Poutine, le 4 mars 2014, lors d'une conférence de presse à Novo-Ogaryovo (Russie). 
Mkutano wa vyombo vya habari wa rais wa Urusi Vladimir Poutine, March 4, 2014 jijini Moscou (ALEKSEY NIKOLSKYI / RIA NOVOSTI / AFP)

Kauli ya Urusi inatolewa wakati huu ambapo rais wa Marekani Barack Obama akitishia kusitisha ushirikiano wake wa kibiashara na nchi ya Urusi ambapo pia ameshatangaza kusitisha ushirikiano wa kijeshi na taifa hilo kufuatia hatua yake ya kuivamia nchi ya Ukraine.

Urusi inasisitiza kuwa inauwezo wa kusimama yenyewe hata bila ya kutegemea wafanyabiashara toka nchini Marekani.

 
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry amewasili nchini Ukraine jumanne hii ambapo atakuwa na mazungumzo na utawala wa mpito wa taifa hilo ambao wameomba msaada toka jumuiya ya kimataifa.
 
Ziara ya Kerry inafuatia ziara kama hiyo ambayo imefanywa hapo jana na waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague ambao wote kwa pamoja wanalenga kusisitiza kutoridhishwa kwao na namna ambavyo Urusi imeivamia kijeshi nchi ya Ukraine.
 
Tayari waziri mkuu mpya wa Ukraine, Arseni Iatsenuik ametoa matamshi mengine kukashifu utawala wa Urusi na kuionya kuhusu kuendelea kusonga mbele kwa vikosi vyake kwenye mji wa Crimea.
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s