CHADEMA WASAKA WA KUMPAMBANISHA NA MTOTO WA KIKWETE..

 

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza mchakato wa kutafuta mgombea wa kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Chalinze, ambapo jana fomu za kuwania nafasi hiyo kupitia chama hicho zilianza kutolewa.
 
Katibu Uenezi wa Halmashauri ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye.Photo credits:dewjiblog.com

 
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishaanza mchakato wa kutafutia mgombea wa kuwania nafasi hiyo, ambapo Ridhiwani Kikwete, alishinda kura ya maoni ya wanachama wa chama hicho na sasa anasubiri uamuzi ya vikao vya juu vya chama hicho.
 
Akizungumza na mwandishi jana, Ofisa Uhusiano wa Chadema, Tumaini Makene, alisema fomu hizo zinatolewa na kurejeshwa katika ofisi za Kanda ya Pwani ya chama hicho.
 
“Baada ya kurejesha fomu, walioomba kuwania nafasi hizo watapigiwa kura ya maoni na wanachama wa Chadema wa eneo husika, na baada ya hapo uamuzi wa mwisho utakuwa ni wa vikao vya juu,” alisema Makene.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Uenezi wa Halmashauri ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, alisema bado chama hicho kipo kwenye mchakato wa kuandaa vikao vya juu, vitakavyoyachuja majina ya waliopigiwa kura za maoni na kuteua mgombea wa ubunge kupitia chama hicho.
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s