HOFU YATANDA BUNGE LA KATIBA KUVUNJIKA

Na Daniel Mjema, Mwananchi

Dodoma. Mjadala wa namna ya kuamua Rasimu ya Katiba umezua hofu ya Bunge Maalumu la Katiba kuvunjika.
 
Hashim Rungwe akichangia jambo wakati wa moja ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma. 

Bunge hilo limeangia siku ya 21 kati ya 70 likiwa katika mjadala wa kupitisha kanuni, huku kukiwa na mabishano kuhusu namna ya kupitisha ibara. 
 
 Hadi sasa Bunge hilo limeshapitisha kanuni 85 za uendeshaji wa chombo hicho, ispokuwa mbili tu, ikiwamo ya upigaji wa kura katika kupitisha vipengele mbalimbali katika rasimu, ambayo inaonekana kusababisha mgawanyiko mkubwa.
 
Hali ya kutokubaliana katika masuala kadhaa ilisababisha baadhi ya wajumbe kumtaka Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho aeleze iwapo Bunge hilo lingeendelea au la kutokana na utata wa kisheria na kikanuni kuhusu ibara na sura zitakazokataliwa na wajumbe kwa kura.
 
Akichangia mjadala wa kanuni mjumbe, Dk. Francis Michael aliitaka Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele vyenye ushindani ikae chini na kutoa ufumbuzi kuhusu utata huo.
 
“Inabidi tuwe na uamuzi, hapa tunataka Katiba Mpya au hapana. Hapa tunatumia fedha za walipa kodi. Kuna hoja ambazo zinaonyesha kabisa kuwa zikifika hapa zitagonga ukuta,” alisisitiza.
 
Dk. Michael alipendekeza wanasheria na wakuu wa Serikali wa pande zote za Muungano kutafuta suluhisho mapema.
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s