MWANDISHI UINGEREZA AJA KUONA VITA DHIDI YA UJANGILI

 

Dar es Salaam. Serikali imeanza juhudi za kujinasua kwenye lawama kwamba haifanyi juhudi za kutosha kupambana na ujangili kwa kuwaalika waandishi wa habari wa kimataifa ili kujionea kazi inayofanyika.
 
Mwandishi huyo jana alitembelea ghala la meno ya tembo yaliyohifadhiwa katika Wizara ya Maliasili na Utalii kumwonyesha juhudi ambazo zimekuwa zikifanyika kupambana na ujangili nchini.PICHA|MAKTABA
 
Tayari mwandishi wa Habari wa Uingereza aliyeandika habari katika Gazeti la Daily Mail, Martin Fletcher kuwa Tanzania haifanyi jitihada zozote kukabiliana na ujangili amewasili nchini.
 
Mwandishi huyo aliandika habari kwenye gazeti hilo toleo la Februari 8 na 9, mwaka huu kwamba Serikali ya Tanzania imeshindwa kutimiza wajibu wake katika kuwalinda faru na tembo ambao wako hatarini kutoweka.
 
Mwandishi huyo jana alitembelea ghala la meno ya tembo yaliyohifadhiwa katika Wizara ya Maliasili na Utalii kumwonyesha juhudi ambazo zimekuwa zikifanyika kupambana na ujangili nchini. Akizungumza muda mfupi baada ya kuona ghala hilo, Fletcher alisema ni jambo jema kwa kuwa ameona sehemu ya hazina hiyo.
 
“Nimeona kwa sehemu kubwa hifadhi iliyopo, bado ninaendelea kufuata utaratibu kwa kuwa nimealikwa, siwezi kusema lolote kwa sasa,” alisema Fletcher. Kwa mujibu wa ratiba, leo atapelekwa katika Mbuga ya Selous ambako atajionea ‘utajiri wa wanyama kwenye mbuga hiyo’.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikutana na mwandishi huyo lakini akakanusha kuwa Serikali imemwalika, akisema hiyo ilikuwa ni sehemu ya mpango wake akitaka kujionea mambo yanayotendeka nchini kuhusu suala la ujangili.
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s