RED CROSS YAPIGWA JEKI KUWASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO KILOSA

 

Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale,  akifurahia jambo wakati akipokea mfano wa hundi ya Shilingi Milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii” Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule. Fedha hizo zimetolewa kwa chama hicho kwa ajili ya kuimarisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro na kuacha mamia ya kaya bila makazi. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Julius Kejo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalimu.
Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale,  akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) punde baada ya kupokea msaada wa fedha, kiasi cha Shilingi milioni kumi kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii”Vodacom Foundation” kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Pamoja nae katika picha kutoka Kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.
Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale na Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzanaia”Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule, wakimsikiliza mmoja wa Maafisa wa Tanzania Red Cross punde baada ya kupokea msaada wa fedha kiasi cha Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na Vodacom Tanzania kupitia kitengo hicho  kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro
Mkuu wa Kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania” Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule akizungumza na  waandishi wa Habari (Hawapo pichani) punde baada ya kutoa msaada wa fedha kiasi cha Shilingi milioni kumi Kilichotolewa na kitengo hicho”Vodacom Foundation”kwa ajili ya kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. Pamoja nao katika picha ni Rais wa Tanzania Red Cross, Dr. George Nangale (katikati)Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.

Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania”Vodacom Foundation” Yessaya Mwakifulefule akizungumza na baadhi ya maafisa wa Tanzania Red Cross, punde baada ya kufanya makabidhiano ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni 10 ambazo zitasaidia kuimalisha huduma na kusaidia waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Red Cross yapigwa jeki kuwasaidia wahanga wa mafuriko Kilosa

Dar es Salaam, Tanzania Red Cross  leo imepokea msaada wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kuiwezesha kuimalisha huduma na kusaidia waaliokumbwa na maafa ya mafuriko wilayani kilosa Mkoani Morogoro.

 Itakumbukwa kwamba mnamo tar. 22-23,Januari 2014, mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kutokea ndani ya kipindi cha miaka 15, yalikumba wakazi wa eneo la Dumila, kuwaacha mamia ya wakazi wakiwa hawana sehemu za kuishi, chakula cha uhakika huku miundombinu mbali mbali ya kiuchumi na kijamii ikiwa imeharibiwa vibaya.

Tathmini iliyofanywa na Serikali ya Mkoa wa Morogoro inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 9,000 waliathirika kwa namna na viwango mbalimbali. Mafuriko haya ya ghafla (Flash Flood) yalisababishwa na mvua zilizonyesha katika nyanda za juu za mikoa ya jirani ikiwemo Dodoma, Tanga na Manyara.   Wilaya ya Kilosa ndiyo iliyopata madhara makubwa zaidi kutokana na janga hili ambapo takribani watu 7,600 waliathirika na nyumba zaidi ya 500 kubomoka kabisa na hivyo  familia husika kukosa nyumba za kuishi.  Wilaya nyingine  zilizoathirika ni pamoja na Gairo (waathirika 958), Mvomero (690) .

 Akizungumza wakati wa makabidhiano wa msaada huo Mkuu wa Kitengo cha mfuko wa kusaidia jamii “Vodacom Foundation” Bw. Yessaya Mwakifulefule alisema kuwa matumaini ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dumila yapo kwetu sisi watanzania kujitoa kwa hali na mali kuwarejeshea maisha yao ya awali.

“Kwa kuitambua Tanzania Red Cross kwa majukumu yake katika kuisaidia jamii kwa kukabiliana na maafa, leo tunakabidhi kiasi hiki cha fedha kwa chama cha msakaba mwekundu nchini kuhakikisha dhamira yake ya kusaidia umma wa watanzania katika wakati mgumu kama huu.” Alisema Mwakifulefule

 Rais wa Tanzania Red Cross, Dr.George Nangale, amesema baada ya maafa hayo, chama kilichukua hatua za haraka kwa kutoa msaada wa mahitaji ya dharura kama vile, vyandarua (300), mablanketi (300) na ndoo za maji (300) na madumu ya maji (160) Msaada huu wa awali uliwafikia walengwa katika kipindi cha saa 24 baada ya maafa kutokea.

“Bada ya maafa hayo, chama kilichukua hatua za haraka kwa kutoa msaada wa mahitaji ya dharura kama ilitolewa katika kipindi cha saa 24 baada ya maafa kutokea. Kilichofuata ni tathimini ya awali iliyoonyesha kwamba mbali na mahitaji mengine, makazi ya dharura yalikuwa hitaji muhimu na haraka kutokana na ukweli kwamba familia nyingi zilipoteza nyumba zao” amesema Nangale.

Aliendelea kusema kwamba kwa ufadhili wa shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu Duniani(IFRC), Tanzania Red Cross imeweza kujenga nyumba za dharura kwa ajili ya familia 400 zilizokuwa na uhitaji mkubwa .

Nangale aliendelea kusema kwamba makazi haya ya muda yamegharimu kiasi cha jumla ya shilingi 80,000,000/=(Milioni Themanini).  Mahitaji mengine yanayoendelea kutolewa ni pamoja na magodoro (800), vyombo vya jikoni (seti 400), madumu ya maji (500) sabuni za kufulia, vyandarua, mablanketi, huduma za ushauri/ nasaha(pysco social support), na elimu ya afya na mazingira, vyote hivi vikiwa na thamani ya  takribani shilingi 96,600,000/=. Ufadhili huu umetolewa na IFRC,Shirika la Umoja wa Maitaifa la UNICEF na kampuni Vodacom.

 “Tunawashukuru sana Vodacom na wengine wote waliotuwezesha katika harakati za kutimiza wajibu wetu kwa jamii hasa katika wakati huu wa maafa yaliyotokea huko Morogoro.  Tunatoa wito kwa Taasisi mbalimbali pamoja na watanzania wote kwa ujumla kujenga na kuendelea na moyo wa kupenda kusaidia pale yanapotokea maafa kama haya na mengineyo”, amesema Rais wa Tanzania Red Cross.

 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s