Miaka 20 baada ya Mauwaji ya halaiki Rwanda

 

Katika wakati ambapo Rwanda inatafakari miaka 20 baada ya mauwaji ya halaiki, taasisi ya wanasheria ya Ufaransa imefanikiwa kumhukumu mmojawapo wa waandalizi wa mauaji hayo ya halaiki Pascal Simbikangwa.
 
Majeneza ya wahanga wa mauwaji
 
Kesi ya kwanza ya mnyarwanda aliyekuwa akituhumiwa kuhisika na mauwaji ya halaiki ni hatua muhimu kwa jopo hilo maalum la mjini Paris linaloshughulikia masuala ya aina hiyo na ambalo linaanza kupanua shughuli zake-anasema naibu mwendesha mashtaka mkuu Aurélia Devos.
 
Pascal Simbikangwa,myarwanda wa kwanza kuhukumiwa nchini Ufaransa kwa makosa ya kushiriki katika mauwaji ya halaiki ya watu wa kabila la tutsi mnamo mwaka 1994,alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela Marchi 15 iliyopita,na kuipatia jaza ya kwanza taasisi hiyo inayoshughulikia masuala ya mauwaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinaadamumbele ya mahakama ya mjini Paris.
 
Ikiundwa mapema mwaka 2012,taasisi hiyo imejiwekea lengo la kupambana dhidi ya mitindo ya kutoandamwa kisheria wahalifu wa vita ambao wamekimbilia nchini Ufaransa nchi yenye idadi kubwa ya wahamiaji.
 
“Ni hatua muhimu” amesema Aurélia Devos ambae ni mkuu wa taasisi hiyo ya masuala ya sheria.”Kesi dhidi ya Pascal Simbikangwa imebainisha kwa mkumbo mmoja kwamba ni halali na ni jambo linalowezekana kumfikisha mahakamani nchini Ufaransa mgeni yoyote,kwa makosa aliyoyafanya katika pembe nyengine ya dunia.”
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s