JESHI LA MAGEREZA KUINGIA USHIRIKIANO RASMI NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

PIX 1 (2)Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara alipowasilishwa katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (kulia).

PIX 2 (3) Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (wa tatu)  wakisani hati za makubariano ya ushirikiano kati ya Taasisi hizo mbili.  Wakwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa na wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango anayeshughulikia Teknolojia na Huduma za Kujifunzia Chuoni hapo.
PIX 3 (3) Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa(wa kwanza kulia) na Prof. Modest Valisango (wa kwanza kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
PIX 6 (2) Baadhi wa washiriki wa hafla ya utiwaji sahini makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu cha Huria cha Tanzania wakifuatilia kwa karibu simulizi za  aliyewahi kuwa mfungwa Bw. Haruna Pembe (hayupo pichani) alivyosoma na kumaliza shahada yake ya sharia na hivi sasa anasoma shahada ya uzamili chuoni hapo.

Na Insp Deodatus Kazinja, PHQ

Jeshi la Magereza nchini limeingia katika Makubaliano rasmi na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumatatu 02 Juni, 2014 katika  Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Chuo hicho kilichoko eneo la Biafra Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wajumbe mbalimbali kutoka Chuoni hapo, Jeshi la Magereza pamoja na wanahabari Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tolly Mbwete amesema kuwa ushirikiano kati ya Magereza na OUT umekuwepo kwa muda mrefu ila hivi sasa ni kuuimarisha zaidi kwa kufanya mapitio kwenye maeneo ya ushirikiano kwa lengo kujumuisha maeneo mengi zaidi.

Ametaja maeneo yanayokusuduiwa katika makubaliano hayo kuwa ni Mafunzo na shughuli za utafiti, uandaaji wa mitaala na vifaa vya mafunzo hususani ni katika suala la urekiebishaji wa wahalifu, utoaji wa elimu kwa umma kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hizi mbili, ubadilishanaji wa nyaraka, vitabu vya rejea na vifaa muhimu vya maktaba, maendelea ya kitaaluma kwa watumishi wa Jeshi la Magereza na wafungwa nakadhalika.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja amesema kwa muda wote Jeshi la Magereza limekuwa tayari kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kutoa vibali mbalimbali kwa wanafunzi na wakufunzi wanaotaka kufanya tafiti katika maeneo ya Magereza, kutoa vibali kwa watumishi wa Jeshi la Magereza kusoma katika chuo hicho na kutoa ushirikiano wa dhati kwa wafungwa wanaotaka kusoma kwa kutumia chuo hicho wakiwa gerezani.

Makubaliano haya ya leo yatakuwa ya msaada sana kwa Jeshi la Magereza katika kulifanya liwe la kisasa na kulipunguzia matumizi” Alisema Kamishna Minja.

Katika hafla ushuhuda wa wafungwa kusoma na kufanikiwa wakiwa gerezani ulitolewa na ex-mfungwa Haruna Pembe aliyepata shahada ya sheria (LLB) akiwa gerezani na sasa yuko nje baada ya kushinda rufaa yake akiwa sasa anafanya shahada ya pili ya sheria katika Chuo Kikuu hicho. (Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja, PHQ)

 
Advertisements