NI KWELI BILA UKAWA BUNGE LA KATIBA HALITAATHIRIKA?

Kikundi cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Wakati vikao vya Bunge Maalum la Katiba vikiendelea tena mjini Dodoma wiki hii bila ya kuwepo kwa kikundi kinachojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samweli Sitta amesema amekuwa akisisitiza kuwa bunge hilo halitaahirisha shughuli zake hadi hapo muda wa siku 60 waliopewa utakapokamilika.

Sitta alisema rasimu hiyo ina mambo mengi mazuri lakini pia akasema kuna mambo mengine yanatakiwa kufanyiwa marekebisho ili Watanzania waweze kupata katiba bora.

Ni kweli kwamba maudhui ya rasimu ya katiba yanajumuisha baadhi ya mambo yafuatayo; kuimarisha Muungano wetu kwa kuleta uwiano bora wa mamlaka ya Zanzibar na…

Kikundi cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Wakati vikao vya Bunge Maalum la Katiba vikiendelea tena mjini Dodoma wiki hii bila ya kuwepo kwa kikundi kinachojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samweli Sitta amesema amekuwa akisisitiza kuwa bunge hilo halitaahirisha shughuli zake hadi hapo muda wa siku 60 waliopewa utakapokamilika.

Sitta alisema rasimu hiyo ina mambo mengi mazuri lakini pia akasema kuna mambo mengine yanatakiwa kufanyiwa marekebisho ili Watanzania waweze kupata katiba bora.

Ni kweli kwamba maudhui ya rasimu ya katiba yanajumuisha baadhi ya mambo yafuatayo; kuimarisha Muungano wetu kwa kuleta uwiano bora wa mamlaka ya Zanzibar na Tanzania Bara ndani ya Muungano, kuimarisha haki za binadamu na kuzuia wachache kufuja rasilimali za taifa.

Naamini upo ukweli kwamba ndani ya rasimu hiyo inayojadiliwa yapo mapungufu kwa kuachwa masuala ya kuwezeshwa kuundwa kwa Serikali za Mitaa, maelekezo ya matumizi ya ardhi na rasilimali nyingine.
Hakika kitendo kinachofanywa na wajumbe wa bunge hilo wanaounda Ukawa ni kibaya kwani kususia kikao si jambo jema na badala yake wangelumbana kwa hoja ndani ya bunge.

Niwaombe tu wana Ukawa kwamba waache kupotosha umma na kuonekana kuwa wao ni bora zaidi ya wajumbe wengine walioko ndani ya Bunge Maalum la Katiba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Amir Kificho tayari amewasilisha mapendekezo ya kanuni 12 ambazo zitaliwezesha bunge hilo kukamilisha kazi yake katika muda uliopangwa wa siku 60.

Mapendekezo hayo yalipitishwa katika moja ya kikao cha jioni wiki iliyopita kwa kauli moja kutoka kwa wajumbe waliokuwepo na hivyo kazi ya kuanza kujadili sura zilizobaki zikaanza na zitaendelea wiki hii.

Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba awali akichangia mapendekezo hayo, mjumbe wa bunge hilo na Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangala alisema kuundwe kanuni itakayowabana wajumbe waliotoka katika Bunge hilo na hata wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba iliyoshughulikia mchakato wa ukusanyaji maoni kutoingilia mwenendo wa bunge hilo wakati huu vikao vyake vinapoendelea.

Ni jukumu la wapenda amani wote katika nchi hii kuwahimiza Ukawa kuingia katika meza ya maridhiano kwa sababu muda bado upo na ni vizuri sana wakaingia sasa bungeni kwa sababu yanayojadiliwa yanawagusa wananchi katika majimbo yao moja kwa moja.

Nizidi kumuomba Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe kuliona hili na kukumbuka wahenga waliosema kuwa hakuna vita inayokwisha nje ya meza ya mazungumzo. Hii ni hoja yangu, muitafakari tafadhali. Wanachi wote wanataka Katiba mpya itakayodumu miaka 50 ijayo.Chanzo:www.globalpublishers.info

Leave a comment