MJUMBE WA BARAZA LA KATIBA ALIYEPIGWA AFUATWA WODINI KUPIGA KURA

 

 
 
Na Sharon Sauwa Dodoma. 
 
Mbunge aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Thomas Mgilo baada ya kupigwa na watu wasiojulikana amefuatwa hospitalini ili apige kura kupitisha baadhi ya sura za rasimu. 
 
Tukio hilo limekuja kukiwa na taarifa kuwa baadhi ya kamati zinashindwa kupiga kura kuamua au kuchelewa kuanza vikao vyake kutokana na tatizo la akidi.
 
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge Maalumu, idadi ya wajumbe wanaotakiwa ili kuruhusu kikao kuanza ni nusu ya wajumbe wote, wakati theluthi mbili inatakiwa wakati wa kupiga kura. 
 
Jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba 12, Thuwayba Kisasi akiwa ameongozana na polisi walimpelekea karatasi za kupiga kura Mgilo na alipiga kura ya wazi kuamua kuhusu Ibara ya 39 ya Sura ya Nne ambayo pamoja na mambo mengine, inazungumzia haki za mtuhumiwa au mfungwa. 
 
 Ibara hiyo inataka kutoa ruhusa kwa wafungwa wenye ulemavu kuingia na magongo yao kifungoni, jambo ambalo Mgilo alilipinga. Alisema hawezi kuunga mkono wafungwa wenye ulemavu kwenda na magongo gerezani kwani wanaweza kuyatumia kuwadhuru wengine. 
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s