Hoja za Jaji Warioba mateso Bunge Maalumu

 

 
Na Neville Meena 
 
 Dodoma. Kero za Muungano na taasisi zake zilizotajwa na mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba zimekuwa zikiwatesa wajumbe wa Bunge Maalumu katika mijadala ya rasimu ya Katiba inayoendelea kwenye kamati za chombo hicho. 
 
 Miongoni mwa maeneo ambayo yametajwa kusababisha mvutano mkali katika kamati nyingi ni muundo wa Bunge ambao ulitajwa na Jaji Warioba wakati akiwasilisha taarifa ya Tume kuwa una kasoro nyingi ambazo zimesababisha malalamiko kutoka kila upande wa Muungano.
 
 Habari kutoka katika vikao kadhaa vya kamati zinasema baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao walikuwa wakiamini katika muundo wa serikali tatu pamoja na baadhi wa Kundi la 201, wamesimama kidete wakitaka yafanyike mabadiliko makubwa ya muundo wa Bunge la Muungano.
 
“Muundo wanaopendekeza ni kuwa na Bunge la ‘tatu ndani ya moja’ kwa maana kwamba Spika anakuwa mmoja, lakini huku ndani kunatolewa fursa za wabunge wa Tanzania Bara kunapokuwa na masuala yao na wale wa Zanzibar wakutane kwa masuala yao na yale ya muungano basi wote tukutane,” alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati Namba Tano. 
 
Ikiwa pendekezo la muundo wa aina hiyo ya Bunge utakubaliwa, majimbo ya Zanzibar yatakuwa na mwakilishi mmoja mmoja, tofauti na sasa ambapo kila jimbo lina mbunge anayeshiriki katika Bunge la Muungano na mwakilishi anayeingia katika Baraza la Wawakilishi. 
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s