JK aitisha Kamati Kuu

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu kitakachofanyika Dodoma kesho. 
 
 Habari za uhakika zilizopatikana Dar es Salaam jana, zinasema moja ya ajenda kubwa inayoweza kutawala kikao hicho ni mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba ambalo limesusiwa na wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
 
 Kwa muda sasa Ukawa wamekuwa wakimtaka Rais Kikwete aliahirishe Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma, kwa kile wanachodai kutotendewa haki.
 
Rais Jakaya Kikwete
 
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya CCM kililiambia MTANZANIA kuwa kikao hicho cha siku moja kitajadili masuala mbalimbali likiwamo kufuatilia mwenendo wa makada wa chama hicho ambao katika siku za hivi karibuni kwa namna moja au nyingine wanadaiwa kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
“Nakwambia hakuna mjumbe hata mmoja anayejua nini kinakwenda kujadiliwa, Rais Kikwete amekwenda na siri nzito moyoni…tusubiri tuone nini kitatokea Dodoma. “Hata hivyo, ajenda kubwa itakuwa uamuzi mpya juu ya hatima ya sasa ya Bunge Maalumu la Katiba ambalo mwenendo wake umekuwa ukilalamikiwa na wengi,” kilisema chanzo hicho kutoka ndani ya CCM Makao Makuu. 
 
 Chanzo hicho kilisema kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM kilichoanza juzi mjini Dodoma kufuatilia mwenendo wa makada sita waliopewa adhabu ya mwaka mmoja kwa kuanza kampeni za kuteuliwa kuwania urais kabla ya wakati. Kikao hicho kitatoa taswira na mwelekeo mpya ndani ya CCM. 
 
Uamuzi wa Rais Kikwete kuitisha CC unatokana na uamuzi wa Kamati Kuu iliyoketi Julai 16 mwaka huu ambayo ilipokea taarifa za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonyesha nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais. 

 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s